Waziri wa ElLmu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Uombaji Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi HESLB, Prof. Hamisi Dihenga. Hafla hiyo imefanyika leo Jumanne Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uombaji mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta (TPC), Macrice Mbodo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uombaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Angela Anatory akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uombaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uombaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Prof. Hamisi Dihenga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uombaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam.  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (ZHELB) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uombaji mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uombaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 12, 2022 Jijini Dar es Salaam. Wakuu wa Taasisi kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Shirika la Posta Tanzania (TPC) na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao ni wadau wa kimkakati wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati wa uzinduzi wa mwongozo wa uombaji mikopo kwa mwaka 2022/2023.


************************

Na Magrethy Katengu

Serikali imetenga TZS 573 bilioni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2022/2023zitawanufaisha wanafunzi 205,000 kujiendeleza kielimu na kutimiza ndoto zao.

Akizungumza leo Dar es salaam Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda katika hafla ya Uzunduziwa Mwongozo wa uombaji utakawawezesha wanafunzi wa hao kuomba mikopo amesema kati ya fedha hizo zilizotengwa billion 570 kwa ajili ya mikopo na billion 3.0 zimetolewa kamba ruzuku/Skolaship kwa wananafunzi wenye ufaulu mkubwa katika kozi za masomo ya Sayansi.

"Kwa mwaka wa masomo 2021/2022,ilitenga TZS 570 billion kwa ajili ya mikopo wanafunzi wa Elimu ya kuwanufaisha wanafunzi 177,800 huku mwaka huu ilitenga bilioni 573 na kunufaisha wanafunzi 205,000"amesema ProfMkenda

Hata hivyo amesema Mwongozo huo kuanzia Julai 12-18,2022 utapatikana katika lugha ya kingereza na kiswahili katika tovuti (www.heslb.go.tz)(www.moe.go.tz) kumwezesha wanafunzi mwombaji kuusoma.

"Julai 19-Septemba 30,mwaka huu dirisha la kuomba Mkopo kwa njia ya mtandao litakuwa wazi takribani siku 70 ili kupokea maombi huku uendeshaji wa Programu za elimu kwa waombaji mikopo watarajiwa kufanyika katika Kambi 19 za JKT kupitia vipindi katika vyombo vya habari ikiwemo redio televisheni na mitandao ya kijamii kuanzia Julai 20-Septemba 30 mwaka huu" alisema Waziri

Sanjari na hayo ameelekeza bodi ya mikopo kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu wakishirikianna na taasisi za kiserikali ikiwemo Shirika la Posta,Ritha,Tasafu Ili kuepuka malalamiko kwani ya wanafunzi.

Sambamba na hayo amesema mwa mwaka huu wanafunzi wanaosomea somo la Kiswahili na Lugha watapewa kipaumbele cha kupewa Mkopo kwani imeonekana kuna uhitaji mkubwa ndani na nje ya nchi wakalimani wa Lugha ya kiswahili hivyo Rais ameiomba wapewe kipaumbele hicho wale waliopata alama za juu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo Abdu-Razaq Badru amesema waombaji mikopo waanze michakato mapema ya kwa kuambatanisha nyaraka zao ili kama kutakuwa na changamoto yeyote ile ishughulikiwa mapema kwani ikitokea mtu ucheleweshwaji kufanya mchakato mapema na mwanafunzi anapopata changamoto ya kuhitaji marekebisho inakuwa vigumu kushughulikia .

Aidha kwa mwaka wa fedha 2021/2022 lengo lilikuwa ni kukusanya TZS 182.0 bilioni hadi Juni 30 mwaka huu Jumla ya fedha 183.8 billion zimeshakusanywa hiyo ni sawa na asilimia 32.2 ya fedha iliyotolewa na Serikali kuwakopesha wanafunzi katika mwaka huo masomo