Gari hiyo ndogo aina ya KP A72eV yenye muundo wa Pickup imezindiliwa jana Aprili 2, 2022 jijini Dar es Salam.
Tayari pongezi nyingi zimeanza kutolewa ambapo Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amesifu hatua hiyo na kusema, "Kwangu hapa ni mahali pazuri saana pa kuanzia. Hongera saana Ndugu yetu Masoud Kipanya umeonesha njia. Nategemea kuona mamlaka za ubunifu zikikaa naye na kuangalia namna nzuri ya kuboresha wazo lake na zaidi kufikiri namna bora ya kuwezesha wazo hili kuzaa matunda kwa kuongeza tija kwa mbunifu, Watanzania na Tanzania kwa ujumla." Daniel Chongolo, Katibu Mkuu wa CCM.
Naye Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe. Togolani Mavura naye hamkuwa nyuma kutoa pongezi zake.
"Hongera sana Kaka Masoud Kipanya unazidi kuthibitisha hazina yako ya vipaji, ubunifu na usanifu. Naiona hii ni hatua ya kwanza kuelekea kwenye hatua kubwa kubwa na nyingi mbeleni." ameandika kwenye ukurasa wake wa tweeter.
Masoud Kipanya.
No comments :
Post a Comment