Friday, February 4, 2022

MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO AWASILI NCHINI ETHIOPIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 04 Februari 2022 akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole uliopo Addis Ababa, Ethiopia na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano. Makamu wa Rais yupo nchini Ethiopia  kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaotarajiwa kufanyika tarehe 5 na 6 Februari 2022.

No comments :

Post a Comment