Thursday, October 28, 2021

TOTAL YAZINDUA STARTUPPER CHALLENGE MSIMU WA TATU


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TotalEnergies, Jean-Francois Schoepp (katikati,) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2021 wakati wa kuzindua msimu wa tatu wa shindano la Startupper of the year Challenge inayofadhiliwa na Kampuni ya mafuta ya magari nchini ya TotalEnergies kwa mwaka 2021, 2022. Kulia ni Meneja mahusiano ya kampuni ya Mafuta ya magari ya TotalEnergies, Getrude Mpangile na kushoto ni Meneja mawasiliano wa kampuni ya TotalEnergies, Jamila Tindwa.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TotalEnergies, Jean-Francois Schoepp wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2021 wakati wa kuzindua msimu wa tatu wa shindano la Startupper of the year Challenge inayofadhiliwa na Kampuni ya mafuta ya magari nchini ya TotalEnergies kwa mwaka 2021, 2022. Kulia ni Meneja mahusiano ya kampuni ya Mafuta ya magari ya TotalEnergies, Getrude Mpangile na kushoto ni Meneja mawasiliano wa kampuni ya TotalEnergies, Jamila Tindwa.




KAMPUNI Ya mafuta ya TotalEnergies Market Tanzania Ltd imezindua rasmi msimu wa tatu wa shindano la kitaifa la Startupper kwa mwaka 2021/2022 lenye lengo la kuwatambua, kuwazawadia na kuwawezesha wajasiriamali wachanga ambao wameanzisha biashara zisizozidi miaka mitatu na zenye matokeo chanja kwa jamii ya kitanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa shindano hilo leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Jean-Francois Schoepp amesema shindano la awamu hii litawawezesha kifedha vijana wajasiriamali walio na umri wa 18 hadi 35 ambao wanaendesha miradi ya kibiashara isiyozidi miaka mitatu katika sekta yoyote ya kiuchumi.

''Washindi watachaguliwa kwa kuzingatia; Mradi bora unaowezesha kuanzisha biashara nyingine, Biashara bora isiyozidi miaka mitatu pamoja na mjasiriamali bora wa kike...na dirisha la usajili litafunguliwa rasmi Novemba 4 hadi Desemba 23 mwaka huu, Nawahamasisha vijana wajasiriamali kufuatilia mwenendo wa mashindano haya kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii ya Instagram, Facebook na tovuti yetu ya TotalEnergies Tanzania.'' Amesema.

Kuhusiana na vigezo vya shindano hilo Schoepp amesema, shindano hilo ni maalumu kwa vijana wa umri wa miaka 18 hadi 35, watanzania, wajasiriamali na wenye mradi au biashara isiyozidi miaka mitatu.

Aidha amesema, kila mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 20 na kupata fursa mbalimbali ikiwemo kutangaziwa biashara zao na TotalEnergies, kupata mafunzo ya ziada ya ujasiriamali kulingana na ubunifu wa mradi wa biashara zao na kubwa zaidi ni kwa washindi hao watatu ni kuorodheshwa kwenye shindano la Startupper Challenge barani Afrika ili kupata washindi 3 wakuu barani kote.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa mahusiano ya kampuni hiyo Getrude Mpangile amesema, lengo kubwa na TotalEnergies ni kushirikiana na Serikali katika kuongeza kasi ya suluhisho la tatizo la ukosekanaji wa ajira kwa vijana nchini na bara zima kwa ujumla kwa kujenga mawazo ya kibunifu na kusaidia vijana wajasriamali wenye ari.

''Kutokana na mafanikio makubwa ya awamu mbili zilizopita za mashindano haya tulifanikiwa kuwawezesha vijana kama Doreen Noni, Michael Sayi na Prince Tillya ambao walikuwa washindi wa mwaka 2019....Tumerudi tena awamu hii ya tatu nawaomba wanawake tujitokeze tutumie fursa hii adhimu inayodhihirisha nia ya TotalEnergies ya kusaidia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini na kushirikiana na Serikali ya wamu ya sita katika kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana.'' Amesema.

Getrude amesema shindano hilo la kitaifa litasaidia vijana wengine wengi wenye mawazo chanya ya ujasiriamali kuboresha miradi yao kupitia washindi na washiriki wengine watakaoshiriki mashindano hayo ya Startupper Challenge msimu wa tatu wa 2021/2022.




Meneja mahusiano ya kampuni ya Mafuta ya magari ya TotalEnergies, Getrude Mpangile (kulia,) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2021 wakati wa kuzindua msimu wa tatu wa shindano la Startupper of the year Challenge inayofadhiliwa na Kampuni ya mafuta ya magari nchini ya TotalEnergies kwa mwaka 2021, 2022. Kushoto Meneja mawasiliano wa kampuni ya TotalEnergies, Jamila Tindwa.

No comments :

Post a Comment