Wednesday, June 2, 2021

Wajasiriamali wameaswa kulipa kodi

 
*Kulipa kodi kuunga mkono serikali kuweza kupeleka maendeleo

Na Mwandishi Wetu
WAJASILIAMALI Nchini wametakiwa kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kuhakikisha inawaletea maendeleo makubwa wananchi wake pamoja na kuongeza mapato zaidi Nchini.

Wito huo ulitolewa na Mjasiliamali maalufu Charles Sabiniani maarufu kama Lowasa, alipokuwa akizungumza na Wajasiliamali wanaofanya shughuli hizo huko Wilayani Chato Mkoani Geita alipofika kwa ajili ya kusalimia wanachato wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara kwa nyakati tofauti tofauti.

"Nimetembelea wajasiriamali pamoja na dereva bodaboda nikiwa naongea nao nimewapa elimu kuusu ulipaji kodi za Serikari pamoja na sadaka zitolewazo kwenye nyumba za ibada lakini nimewaelewesha kwamba wakiwa na utaratibu wa kulipa kodi wataendelea kufanya shughuli zao kwa uhuru zaidi na bila kubughudhiwa na mtu," alisema Lowasa, na kuongeza;

"Nimewambia wajasiriamali wengi wanakwepa kodi za Serikari ndio maana hawafanikiwi, unapolipa kodi Serikali inatutengenezea Shule, Hospital, Vituo vya Police, Barabara na huduma nyingine nyingi za kijamii ambazo ni kwa manufaa yetu."

Lowasa ambaye pia ni Kada wa CCM alisema kuwa, kutokana na hali hiyo wajasiliamali watakubaliana kwamba kodi wanazolipa pamoja na wafanyabiashara wengine wakubwa zinawapatia watanzania na Taifa kwa ujumla huduma mzuri na zenye kuleta tija zaidi tofauti na pale anbapo kodi hizo zingekuwa zinakwepwa.

"Mfano watu wanapolipa kodi Shule zinajengwa na kwenye shule wanatoka madaktari, wachungaji, wabunge, mashehe na watu wengine wenye taaluma mbalimbali na hawa wakiwa wanashukuru kwa Mungu baraka zinaenda mpaka kwa walipa kodi za serikali." Alisema Lowasa.

Alisema anaamini kwamba Wajasiliamali wanazo changamoto nyingi wanazokumbana nazo ambazo nyingine zimekuwa zikitokana na baadhi yao kukwepa kulipa kodi.

"Mfano mtu anakopa milioni 10 pale pale anatoa sadaka ya shukrani kwa Mungu akija afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hawamwambii ukweli kwenye makadilio kwa mantiki hiyo tayari anakua kaharibu baraka zake kwa kusema uongo hivyo nawaomba muwe makini katika kulipa kodi za Serikari," alisema Lowasa.

Hata hivyo mjasiliamali huyo ambaye pia ni Kada aliwaomba Wajasiliamali hao pamoja na wafanyabiashara kuwa wakati wakiendelea kutekeleza hiyo adhima ya kulipa kodi kwa wakati pia waendelee kumuunga mkono Mama Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake kubwa za kuwaletea maendeleo watanzania na Taifa kwa ujumla.

"Kwenye suala la ulipaji kodi naamini tutakua tunamuunga mkono mama yetu Samia Rais Mwanamke wa kwanza ambae ukifuatilia alitabiliwa miaka ya 1480 lakini pia amekua na Hayati magufuli na Magufuli kwenye kampeini aliwai kusema nimewaletea mama kama sipo mama yupo hivyo mimi kama viongozi wa Taasisi mbalimbali namuunga mkono Mama Rais Samia na kumuombea Baraka tele kama kiongozi.

 

No comments :

Post a Comment