Friday, April 30, 2021

UNDP YATOA KOMPYUTA ZENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 40/=

 

 Mkurugenzi wa Taha Jacqueline Mkindi  akimkabidhi kompyuta 10 zilizotolewa Kama zawadi na washirika wao ambao ni UNDP kwa meneja wa shule ya  sekondari shepherds Lucy Moses tukio lililofanyika hivi katika viwanja vya shule hiyo iliopo Katika kata ya Mlangarini Wilayani Arumeru.
Mkurugenzi wa Taha  Jacqueline Mkindi akiongea na wanafunzi,walimu na baadhi ya wazazi Katika hafla ya kukabidhi komputa 10 zinazotolewa na UNDP kwa shule ya sekondari Shepherds (picha na Woinde Shizza, ARUSHA)

wanafunzi wa shule ya sekondari ya shepherd wakisikiliza kwa makini .

 Na Woinde Shizza, Michuzi Tv


WALIMU wa shule mbalimbali wametakiwa kuwafundisha wanafunzi wao elimu ya natharia na vitendo ili pindi wanapomaliza masomo yao na kwenda mtaani waweze kujiajiri kirahisi na sio kutegemea kuajiriwa 

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa Taha Jackline Mkindi jana wakati akikabibidhi komputa kumi na vifaa vyake venye thamani ya Shilingi milioni 48 vilivyotolewa na washirika wao ambao ni UNDP kwa ajaili ya kuwapatia wanafunzi wa shule ya sekondari Shepherds iliopo katika Kijiji cha Manyire kilichopo katika kata ya Mlangarine

Alisema kuwa kazi ya TAHA ni kuhamasisha na kutangaza sekta ya horticulture nchini ,lakini vilevile pia sekta hii inapendwa sana na vijana,na katika kuhamasisha huku sasa hivi hatuangalii tu vijana ambao wanatoka vyuoni lakini tunataka wale vijana ambao wanatoka kwenye msingi vijana ambao wapo katika levo ya shule za msingi hadi wale waliopo katika shule za sekondari pamoja na wale ambao kabla hawajafika vyuoni.

Alisema kuwa wao kama TAHA wameanzisha mikakati mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule mbalimbali hapa nchini ,ambapo katika kuwagusa hawa vijana ili waweze kuelewa kabisa na kupenda sekta ya kilimo kuanzia wakiwa wadogo.

‘’chanzo cha komputa hizi kuletwa hapa kama zawadi ni kwamba sisi kama Taha tulikuja kutoa elimu ya kilimo cha mboga na matunda kwa wanafunzi hawa wa shule hii ya sekondari ya shepherds baada ya kutoa elimu ,tulikuwa tunawafatilia mara kwa mara n ahata mmoja wa washirika wetu alipokuwa kututembelea ambaye ni UNDP tuliamua kumleta hapa ,alivyokuja na kuona namna wanafunzi hawa wanavyofanya kilimo na kukielezea ,namna uhamasishaji wa watoto hawa ulivyo ndio akaadi kuwapa komputa hizi wanafunzi hawa ili waendelee kujifunza zaidi maswala ya kilimo “alisema Mkindi

Alisema kutokana na mambo ambayo wanayona wanafunzi hawa wanayafanya yamewapa motisha zaidi ya kuendelea kutoa elimu kwa shule zingine na vijana wengine kwani wanafunzi hawa wameonyesha wanauelewa mkubwa wa masomo ya sanyansi na teknolojia jambo ambalo limewashangaza sana pia wana uelewa wa mazao mbalimbali ya kilimo .

Aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa namna wanavyoendelea kuwafundisha wanafunzi hao na kusema kuwa wanawafundisha watoto hao jinsi ya kujiajiri pindi wanapotoka shuleni hapo kwani wanakuwa na elimu ya maarifa na vitendo kwa kilimo na jinsi wanavyoendelea kupewa elimu zaidi ndio itawasaidia wao kuwa wadau wazuri wa kilimo hapo baadae,kwani kilimo ni mti wa mgongo kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu ya Tanzania .

Kwa upande wake mmoja wawanafunzi wa shule hiyo Kennedy Lomboi aliishukuru Taha kwa kuwapa elimu ya kilimo ambapo alisema kuwa wanaimani kabisa pindi watakapo maliza elimu yao ya sekondari wanapoenda nyumba kusubiri matokeo wataendelea kujiajiri kwa kufanya kilimo.

Aidha aliishukuru UNDP kwakuona umuihimu wao na kutambua kazi wanazifanya za kilimo wanapokuwa shuleni hadi wakaamu kuwapatia zawadi ya komputa ambazo alisema kuwa zitawasaidia kuendelea kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo kupitia mitandao mbalimbali

 Kwa upande wake meneja wa shule ya shepherds sekondari Lucy Moses aliwashukuru Taha kwa kumleta mshirika wao ambaye ni UNDPaliyeweza kuwapatia komputa kwa ajili ya wanafunzi waliopo hapo shuleni ambapo aliwahaidi kuzitunza na kuzifanyia kazi wa lengo lililokusudia huku akaiwasihi walimu wa shule zingine kujitahidi kutembelea TAHA na kupata ujuzi ambao utawasadiia vijana kujifunza mbinu mbalimbali za kujiajiri pindi wanapo maliza 
shule na sio kutegemea ajira za serikalini.

No comments :

Post a Comment