Waziri
wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima akikagua mitambo ya kufua hewa tiba
(Oksijeni) iliyosimikwa Kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma.
Waziri
wa Afya akimjulia Hali mmoja wa Watoto waliomo Kwenye wodi
ilivyounganishwa Oksijeni Kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma.
Mmoja
wa Wazazi wa Watoto waliolazwa Kwenye hospitali hiyo akiongea na Waziri
wa Wizara ya Afya Dkt. Dorothy Gwajima wakati alipotbelea wodi hiyo na
kujionea jinsi Oksijeni ilivyounganishwa wodini
Dkt.Gwajima
akinawa mikono Mara baada ya kutoka Kwenye Duka la dawa la tiba asili
lililopo Kwenye hospitali hiyo.Inashauriwa kunawa mikono mara kwa mara
kwa maji tiririka na sabuni.
Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo wakimsikikiza Waziri wa Afya(hayupo pichani.)
Na Catherine Sungura, WAMJW-Dodoma
SERIKALI
imeweza kujibu changamoto za wataalamu wa afya katika hospitali saba za
rufaa za mikoa ili kuwahudumia kwa ufanisi wagonjwa wa dharura kwa
kuimarisha kwa kusimika mitambo ya kufua hewa tiba (Oksijeni) na
hivyo kupunguza gharama za uendeshaji wa hospitali hizo na kuwezesha
hospitali zingine za halmashauri na vituo vya afya.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati alipotembelea hospitali ya rufaa ya
mkoa Dodoma kujionea jinsi walivyounganisha mitambo hiyo kwenye wodi ya
wagonjwa mahututi na watoto.
Dkt.Gwajima
amesema mitambo hiyo ambayo Serikali kwa kushirikiana na Benki Kuu ya
Dunia hivi sasa imefungwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa saba ya
Dodoma, Mtwara ,Manyara, Mbeya, Amana Geita na Songea na hivyo wizara
yake ipo njiani kukamilisha kufungia hospitali zote za rufaa za mikoa
hapa nchini.
“Mitambo
hii imefungwa kwa gharama isiyopungua bilioni 1.4 kila hospitali na
inalenga kuzalisha mitungi 200 ya hewa hiyo kwa masaa 24 , na kila
mtambo unayo sehemu ya mabomba yenye mita 400 yanayosafirisha hewa hii
pia mitungi 73 imenunuliwa pamoja na mitambo hii kwa hivyo, haya ni
mapinduzi makubwa”. Alisisitiza.
Aidha,
Dkt. Gwajima amefurahishwa na uongozi wa hospitali hiyo kwa kukamilisha
kufunga mitambo hiyo na kuanza kutoa huduma kwenye wodi ya wagonjwa
mahututi(ICU) pamoja na wodi ya watoto na hivyo wameweza kuunganisha
vitanda 78 kutoka vitanda 10 vya awali na kufanya jumla ya vitanda 88
kupatiwa huduma hiyo hospitalini hapo.
“Hatua
hii itapunguza kwa kiwango kikubwa gharama za kuhudumia mgonjwa
mwenye mahitaji ya hewa hii. Wito wangu tuitumie vizuri na kuzingatia
na kuhakikisha matengenezo kinga yanafanyika kwa ufanisi”.
Dkt.
Gwajima amesema kuwa uwekezaji huo umeweza kujibu changamoto ya
kipindi cha mlipuko wa Covid-19 ulioripotiwa nchini mwezi Machi mwaka
2020 na hivyo kusababisha kuongezeka kwa mahitaji ya hewa ya oksijeni na
kuwa gharama zake zilipanda.
“Niwapongeze
sana waganga wafawidhi wa hospitali za rufaa za mikoa kwa kuja na wazo
hili la kufunga mitambo hiyo kwenye hospitali zetu na hivyo tutaweza
kusaidia hospitali za wilaya na vituo vya afya na hivyo kuwapunguzia
matumizi ya fedha ya kununua oksijeni, haya ni mapinduzi makubwa kwa
Serikali yetu”. Alisisitiza Dkt. Gwajima
Aliongeza kuwa
Kwa
upande kwa kuepuka magonjwa ya kuambukiza ambayo yameanza kuyakumba
mataifa mengine, Waziri huyo aliwataka waganga wakuu wa mikoa na
wafawidhi kwenye hospitali za rufaa za mikoa kuendelea kutoa elimu kwa
umma kwa kutumia vyombo vya radio vilivyopo kwenye maeneo yao (Community
radio) ili kuwaondolea wananchi hofu na kuendelea kuchukua tahadhari ya
kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza ikiwemo janga la
Corona.
“Serikali
kupitia sekta ya afya kwa kushirikia na wadau wake nchini iko makini
kufuatilia kinachoendela duniani na kuchukua hatua mbalimbali za
kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa salama na imara katika
kudhibiti milipuko ya magonjwa mbalimbali ikiwemo huu wa
Covid-19”.Alisema Dkt. Gwajima.
Dkt.
Gwajima aliwakumbusha wadau,wataalam pamoja na wananchi wote kuendelea
kuchukua tahadhari muhimu ambazo zimekuwa zikielimishwa mara kwa mara
dhidi ya kujikinga na kudhibiti magonjwa mbalimbali ikiwemo C0vid-19
kwa kuepuka hofu, kuimarisha tabia ya kunawa mikono mara kwa mara kwa
maji safi tiririka na sabuni, kufanya mazoezi,kula lishe au vyakula vya
mbogamboga kwa wingi na matunda,kutumia tiba asili, kuepuka misongamano
isiyo ya lazima na mwisho kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za
afya mara unapoona dalili za maradhi yeyote.
Naye
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa Dodoma Dkt. Ernest Ibenzi
amesema wanatarajia kufunga mitambo ya kujazia hewa tiba hiyo ili
kuweza kusaidia vituo vya afya vilivyo jirani na kusambaza huduma hiyo
kwenye hospitali nzima.
No comments :
Post a Comment