……………………………………………………………………………………..
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro
NCAA,imeahidi kuboresha miundo mbinu katika hifadhi zake ili kurahisisha
shughuli za utalii na kuwa rafiki kwa wadau wa utalii wanaosafirisha
watalii kutembelea hifadhi hizo.
Akiongea wakati akijibu matatizo yaliyoibuliwa
na wadau wa utalii katika mkutano wa pamoja uliofanyika jijini Arusha
kamishna msaidizi Mwandamizi wa huduma za utalii, Paulo Sifoo alisema
suala la ubovu wa barabara katika hifadhi zake linashughulikiwa kwa
haraka ili barabara zote korofi ziweze kupitika kwa urahisi katika
kipindi chote Cha mwaka mzima .
“Tunaendelea
kupambana kupitia mpango kazi wetu ili barabara zote zilizopo hifadhini
ziweze kupitika katika msimu wote wa mwaka, nilengo letu kuhakikisha
barabara zetu zinatengenezwa kwa tabaka gumu ili tatizo liweze
kuisha”alisema
Akiongelea suala la
matatizo mengine likiwemo suala la uhaba wa maji hifadhini alisema suala
hilo lipo katika mpangokazi wa NCAA kwa kuanza kuvuna maji ya mvua
baada ya jitihada za kuchimba visima kushindikana kutoa maji.
Katika hatua nyingine
Sifoo ameonya suala la madereva wa utalii wakiwemo wa NCAA wanaokiuka
taratibu za kuendesha gari hifadhini ikiwemo mwendo Kasi ,watachukuliwa
hatua stahiki ikiwemo kutozwa faini Kwa mujibu wa sheria za uhifadhi.
Awali Baadhi ya wadau
hao wa utalii,Msangi Halifa na Ridas Laizer walisema kuwa tatizo kubwa
katika hifadhi ya Ngorongoro ni suala la miundo mbinu ya barabara.
Aidha wadau hao
wameishukuru mamlaka hiyo ya Ngorongoro kwa hatua ya kuzifanyia kazi
Kero mbalimbali zinazolalamikiwa na wadau wa utakii ambazo zimekuwa
zikikwamisha shughuli za utalii katika hifadhi ya Ngorongoro na Olduvai.
No comments :
Post a Comment