Charles James, Michuzi TV
SIKUOTA!
Hii ni kauli ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Philip Mpango baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika
nafasi hiyo leo Ikulu, Chamwino Dodoma.
Dkt.
Mpango amesema nafasi aliyoteuliwa hakuwahi kuiota kuishika ambapo
amemuahidi Rais Samia kuwa hatomsaliti kama ambavyo Yesu alisalitiwa na
mwanafunzi wake Yuda Eskarioti kwa vipande 30 vya fedha.
"Mimi
mtoto wa maskini sikuota kushika nafasi hii, nakuahidi nitatekeleza kwa
bidii kazi zote utakazonielekeza na kazi zingine za katiba kama
ilivyoelekezwa kwenye ibara ya 40, niko tayari kufanya kazi, nitume
usiku na mchana hasa kufanikisha Ilani ya CCM.
Na
katika kutekeleza majukumu hayo yote ntashirikiana na viongozi wote wa
pande zote mbili za muungano, mihimili yote mingine na zaidi viongozi
wengine." Amesema Dkt Mpango.
Makamu
wa Rais Dkt Mpango ambaye alikua ni Mbunge wa Jimbo la Buhigwe ametoa
rai kwa wananchi wa Jimbo hilo kuhakikisha wanamchagua Mbunge
anayetokana na Chama cha Mapinduzi CCM ambaye ataletwa na chama hicho.
"Nishukuru
pia kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama kwa kulipitisha jina langu,
niwashukuru wananchi wangu wa Buhigwe kwa kunipa imani yao kwangu kwa
kunichagua, naamini hiko kibali pia kimetoka kwa Mungu na kimesaidia
wewe Rais kuniteua." Amesema Dk Mpango
No comments :
Post a Comment