Wafanyakazi kiwanda
cha malti super brand wakiwa wanafanya kazi ya kupaki bidhaa tayari
kupelekwa sokoni kama walivyokutwa na kamera ya matukio mjini Babati
picha zote na Ahmed Mahmoud Manyara
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Malti Super Brand David mulokozi akiongea na vyombo vya habari kuhusu kiwanda kinavyozalisha
Moja wa taalam
kiwanda hicho akipnyesha mitambo inavyofanya kazi kama wakati wanahabari
walipotembelea kiwandani hapo mapema mwishoni mwa wiki picha zote na
Ahmed Mahmoud Manyara
…………………………………………………………………………………………………
Na Ahmed Mahmoud Babati
Baadhi ya
wafanyabiashara Mkoani Manyara wameipongeza serikali kwa kuondoa
urasimu katika uwekezaji wa viwanda ,Jambo lililowahamasisha kuanza
ujenzi wa viwanda mbalimbali vya uzalishaji.
Mmoja ya
wafanyabiashara hao ,David Mulokozi ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa
kiwanda Cha kutengeneza vinywaji vikali Cha Mati Super Brands LTD
kilichopo mjini Babati ,ameliambia gazeti hili kwamba Sera ya Rais John
Magufuli ya Tanzania ya Viwanda imemfungua macho na kuamua kuanzisha
Viwanda vya uzalishaji.
“Nilifanikiwa
kufungua kiwanda kimoja Cha pombe kali Mwaka 2017 lakini hadi Sasa
nifungua mefika viwanda vingine vitatu vya pombe Kali na pia nipo mbioni
kufungua kiwanda kingine Cha dawa za binadamu baada ya serikali
kuwatengenezea mazingira mazuri ya uwekezaji”amesema.
Amesema kuwa baada ya
rais Magufuli kuingia madarakani Mwaka 2015 na kuja na sera ya
ujenzi wa viwanda,Jambo hilo lilimhamasisha na kuamua kuanzisha kiwanda
wilayani humo ambacho kimekua na kuzalisha viwanda vingine viwili na
Sasa yupo mbioni kuanzisha kingine Cha dawa za binadamu
Amesema viwanda
hivyo vinazalisha vinywaji vikali aina ya Sed Pineapple Flavored Gin,
Strong Dry Gin , Strong Coffee Flavored Gin New to be Launched na
Tanzanite Premium Vodca.
Amesema kuwa tangu
ameanzisha kiwanda hicho Mwaka 2017 amezalisha ajira zaidi ya 150 huku
akitoa kipaumbele kwa wananchi wanaoishi jirani na kiwanda chake ikiwemo
kuwajengea Mundo mbonu.
“Niliamua kuanzisha
kiwanda nikiwa na mtaji wa shilingi milioni 20 hasa baada ya kuvutiwa na
sea ya Rais Magufuli ya ujenzi wa viwanda ,Sasa hivi mtaji wangu
umekuwa na wala sitegemei mkopo kutoka sekta za fedha “Alisema Mulokozi.
Amefafanua kwamba
kabla ya kuanzisha kiwanda hicho alikuwa ameajiriwa kwenye kiwanda Cha
mtu jijini Arusha kama afisa masoko lakini baada ya rais Magufuli kuanza
kuhamasisha watu kujenga viwanda ,aliamua kuacha kazi na kufungua
kiwanda chake mjini Babati.
“Tuimefungua vituo
vya mauzo katika mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwemo,Arusha,
Kilimanjaro ,Tanga, Dar es Salaam, Morogoro,Mwanza na Mikoa mbalimbali
hapa nchini na nchi jirani ya DRC Kongo,Kenya ,Rwanda,Zambia, Malawi, na
Burundi”Amesema
Ameongeza kuwa
matarajio yake ni kuwa na kiwanda kikubwa kinachoongoza kwa mauzo hapa
nchini na ulipaji mzuri wa Kodi ya serikali.
Amesema Siri ya
mafanikio ni usimamizi na ufuatiliaji pia kuajiri wataalamu wenye ujuzi
,kujua masoko na kuepuka kutegemea mikopo mikubwa katika kuendesha
biashara yako.
Amewashauri
wafanyabiashara wengine kutumia fursa hii ya raisi Magufuli kuanzisha
viwanda na kutoogopa TRA kwani urasimu uliokuwapo hapo awali kwa Sasa
umekwisha.
No comments :
Post a Comment