Sunday, February 28, 2021

RAIS WA ZANZIBAR DK. HUSSEIN ALI MWINYI AZINDUA 'APP' YA SEMA NA RAIS MWINYI

    RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi  akisistiza jambo wakati akizundua APP ya Sema na Rais Mwinyi (SNR MWINYI ) uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika jana usiku 27-2-2021.(Picha na Ikulu)

    BAADHI ya wageni waalikwa katika hafla ya Uzinduzi wa APP ya Sema na Rais Mwinyi  (SNRMWINYI ) uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar jana usiku, wakimsikiliza Mkurugenzi wa RAHISI Bw, Abdulrahman Hassan (hayupo pichani) akitowa maelezo jinsi ya kujiunga na kuwasilisha malalamiko yako kwa Taasisi husika.(Picha na Ikulu)

    KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi kuizindua APP ya Sema na Rais Mwinyi (SNR MWINYI) hafla hiyo imefanyika jana usiku katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

    RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” Unguja Bi. Suzan Kunambi, Mkurugenzi wa Rahisi Bw.Abdulrahman Hassan na Mkurugenzi wa Com.Net.Bw. Mohammed Othman, walipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar kuhudhuria hafla ya Uzinduzi wa APP ya  Sema na Rais Mwinyi ( SNRMWINYI ) iliozinduliwa jana usiku 27-2-2021.(Picha na Ikulu)

    WAGENI waalikwa katika hafla ya Uzinduzi wa APP ya Sema na Rais Mwinyi (SNR MWINYI ) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuizindua APP ya SNRMWINYI, katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar jana usiku 27-2-2021.(Picha na Ikulu)

    RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwenyekiti wa Rahisi Mhe. Toufiq Salim Turky, baada ya uzinduzi wa APP ya Sema na Rais Mwinyi kuwasilisha Kero za Wananchi kupitia njia ya Simu za mikononi kutuma ujumbe wao na kuwafikia wahusika, na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Mkurugenzi wa Rahisi Bw. Abdulrahman Hassan na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama baada ya kuwasili katika ukumbi wa Hoteli ya Verde kuhudhuria Uzinduzi wa APP ya SNRMWINYI, wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Mkurugenzi wa Rahisi.Bw. Abdulrahman Hassan  na Mkurugenzi Com.Net.Bw. Mohammed Othman na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)

No comments :

Post a Comment