Naibu
Waziri wa Ardhi, Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Hati ya Ardhi mkazi wa
Kiegeya mkoani Morogoro, Annet Andrew wakati wa kugawa hati kwa
wananchi wa Yesper, Lukobe na Kiegeya wakati wa ziara ya kukagua
utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro tarehe 30
Desemba 2020. (Picha na Munir Shemweta-WANMM/Diramakini).
Dkt.Mabula ametoa maelekezo hayo Desemba 30, 2020 mkoani Morogoro wakati akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi pamoja na uongozi wa mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara yake ya siku moja kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi pamoja na miradi inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Amesema, Wizara
yake ilifikiri kushirikisha makampuni binafsi katika zoezi la
urasimishaji ingerahisisha kazi ya kupima na kumilikisha wananchi maeneo
yao, lakini matokeo yake baadhi ya makampuni na watu wachache wametumia
nafasi hiyo kufanya ulaghai wa kuchukua fedha za wananchi bila
kukamilisha kazi ya urasimishaji.
Sehemu
ya wananchi wa maeneo ya Yesper, Lukobe na Kiegeya katika mkoa wa
Morogoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi, Dkt.Angeline Mabula
(hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta
ya ardhi katika mkoa wa Morogoro.(Picha na Munir
Shemweta-WANMM/Diramakini).
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mkuu wa
Utawala katika Chuo cha Ardhi Morogoro ameonekana kushirikiana na
watuhumiwa kwa namna moja ama nyingine na uamuzi wa kumsimamisha ni
kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Awali,
Dkt. Mabula alielezwa na Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro, Huruma Lugala
kuwa wakati uongozi wa chuo hicho ukifanya jitihada za kukiboresha chuo
ikiwemo kudhibiti hujuma mbalimbali ilibainia baadhi ya Wakufunzi wake
kujihusisha na kazi ya urasimishaji katika maeneo mbalimbali kwa kutumia
jina la chuo kujipatia fedha.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula
akizungumza na Watendaji wa Sekta ya Ardhi (hawapo pichani) katika Chuo
cha Ardhi Morogoro Desemba 30, 2020 wakati wa ziara yake ya kukagua
utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kukagua miradi inayoendeshwa na
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani Morogoro. (Picha na Munir
Shemweta- WANMM/Diramakini).
Amesema,
chuo chake baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na kubainia
udanganyifu kwa baadhi ya watumishi wake kiliamua kuwasimamisha
Wakufunzi wawili kupisha uchunguzi na kuwataja watumishi hao kuwa ni
Adolf Milungala anayetuhumiwa kujipatia shilingi Bilioni 1.9 na Hamis
Abdalah Kindemile milioni 275 fedha zilizokuwa malipo ya urasimishaji
katika mitaa 43 Morogoro.
Hata
hivyo, Mkuu huyo wa Chuo cha ARIMO amesema wakati uchunguzi ukiendelea
dhidi ya watuhumiwa, Mkuu wa Utawala Lori amekuwa akishirikiana na
watuhumiwa kukwamisha uchunguzi na hata pale alipotakiwa kujieleza kwa
barua alijibu kwa dharau na kuongeza kuwa hata alipoitwa na tume ya
uchunguzi aligoma kwa kisingizo cha ugonjwa.
Naibu
Waziri wa Ardhi Dkt. Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Yesper,
Lukobe na Kiegeya mkoani Morogoro wakati wa zoezi la kugawa Hati ya
Ardhi wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika
mkoa wa Morogoro.(Picha na Munir Shemweta-WANMM/Diramakini).
Naibu
Waziri Mabula ameupongeza uongozi wa Chuo cha ARIMO kwa hatua
ilizochukua za kuwasimamisha watuhumiwa kupisha uchunguzi na kusisitiza
kuwa Wizara yake imeanza kuchukua hatua kwa makampuni yote yaliyoshindwa
kukamilisha kazi za urasimishaji.
"Kufuatia
tukio hili halmashauri inatakiwa kuchukua hatua za kukamilisha upimaji
katika maeneo ambayo watuhumiwa walichukua fedha na nimekiagiza Chuo cha
Ardhi Morogoro kuhakikisha na kinafanya upimaji katika maeneo
hayo,’’amesema Dkt Mabula.
Naibu
Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula akikagua mradi wa ujenzi wa ofisi
ya wilaya ya Wakala wa Misiti Tanzania (TFS) iliyopo wilaya ya Mvomero
wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa
wa Morogoro tarehe 30 Desemba 2020. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero,
Albinus Mugonya.(Picha na Munir Shemweta-WANMM/Diramakini).
Kwa
mujibu wa Dkt Mabula, lengo la Wizara ya Ardhi ni kwamba mwananchi
aliyetoa pesa apimiwe na apate haki yake ya msingi ya kupatiwa hati na
kusisitiza kuwa hilo ni onyo kwa makapuni yote yasiyotekeleza kazi
kuchukuliwa hatua na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mbaula ameonesha kutoridhishwa
na kasi ya ukusanyaji maduhuli ya serikali katika mkoa wa Morogoro
aliyoyaeleza kuwa hadi kufikia Desemba 2020 kiasi cha bilioni 2.3 pekee
kati ya bilioni 11 ndicho kilichokusanywa ikiwa ni sawa na asilimia 18.
Pia
alisema mkoa wa Morogoro unadai takriban Trilioni 1.06 kutoka kwa
wamiliki wa ardhi wasiolipa kodi ya pango la ardhi na kubanisha kuwa
watendaji wa sekta hiyo wamekuwa hawaoneshi juhudi zozote za kudai fedha
hizo wakati wakijua kuna madeni makubwa.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na
Mkuu wa wilaya ya Mvomero Albinus Mugonya wakiangalia sehemu ya
maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wilaya ya Wakala wa Huduma za Misitu
(TFS) iliyopo Mvomero mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya kukagua
utendaji kazi wa sekta ya ardhi.(Picha na Munir
Shemweta-WANMM/Diramakini).
Naibu
Waziri wa Ardhi aliongeza kwa kusema kuwa, Wizara yake kwa sasa itakuwa
ikiwapima wakuu wa idara za ardhi kwenye halamashauri na Maafisa Ardhi
Wateule kwa vigezo vya utendahji ikiwemo makusanyo ya kodi na kusisitiza
watakaoshindwa wataondolewa katika nafasi hizo.
Aidha,
Dkt Mabula katika ziara yake mkoani Morogoro alikagua pia ujenzi wa
mradi wa Ofisi ya Wilaya ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) iliyopo
Mvomero unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).Pamoja na Naibu
Waziri wa Ardhi kuonesha kuridhishwa na ujenzi wa miradi inayojengwa na
NHC katika maeneo mbalimbali alilitaka Shirika hilo kuhakikisha miradi
hiyo inatekelezwa kwa ubora na kwa gharama nafuu.
No comments :
Post a Comment