Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi akipokea Nishani Maalum ya juu ya Mlima Kilimanjaro kutoka kwa
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa, Baba Askofu Mstaafu Elinaza Sendoro
wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho Mjini Iringa.
Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi akionesha Nishani Maalum ya juu ya Mlima Kilimanjaro aliyopokea
kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa, Baba Askofu Mstaafu Elinaza
Sendoro wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho Mjini Iringa.
Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Julius Mbungo akionesha Nishani Maalum
ya juu ya Mlima Kilimanjaro aliyopokea kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Iringa, Baba Askofu Mstaafu Elinaza Sendoro wakati wa Mahafali ya 23 ya
Chuo hicho Mjini Iringa.
…………………………………………………………………………………………………
Na Kanali Juma Nkangaa SIPE, Iringa
Chuo Kikuu cha Iringa
(zamani Tumaini University) kimemtunukia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,
Jenerali Salvatory Venance Mabeyo Nishani Maalum ya Mlima Kilimanjaro
(University of Iringa Miunt Kilimanjaro Award) ambayo hutolewa kwa
Viongozi wa juu Serikalini ambao wametoa mchango wa kutukuka kwa Chuo au
Tasnia ya Elimu kwa ujumla. Tukio hilo limefanyika wakati wa Mahafali
ya 23 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika “campus” ya Chuo Mjini Iringa
tarehe 28 Nov 20.
Mwingine
aliyetunukiwa Nishani hiyo Maalum ya juu wakati wa Mahafali hiyo ni
Mkurugenzi wa TAKUKURU, Brigedia jenerali John Julius Mbungo. Kwa mara
ya kwanza Nishani hiyo ilitunukiwa kwa aliyekuwa Rais (Mstaafu) wa Awamu
ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William
Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakati wa Mahafali ya 22 ya Chuo hicho
mwaka 2019.
No comments :
Post a Comment