Mkuu
wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa NMB - Abella Tarimo (mwenye rasta)
akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Rufaa Iringa (kushoto kwake) Dk. Robert Salim na Mganga
Mfawidhi Dk. Alfred Mwakalebela (kulia)
Mkuu
wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa NMB - Abella Tarimo (mwenye rasta)
akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Rufaa Iringa (kushoto kwake) Dk. Robert Salim na Mganga
Mfawidhi Dk. Alfred Mwakalebela (kulia)
Katika kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja, Benki ya NMB kupitia Mameneja wake wa huduma kwa wateja wa Kanda ya Dar es Salaam, Nyanda za Juu na Kanda ya Ziwa imetoa vifaa mbalimbali vya Afya vyenye thamani ya sh. milioni Tisa, katika mikoa ya Iringa na Kagera ikiwa ni sehemu ya kurudusha kwa jamii.
Mbali
na vifaa hivyo, wafanyakazi wa NMB Tawi la Iringa wametoa vifaa vya
shule kwa wanafunzi wa shule za msingi Mapinduzi, Wilolesi na Saint
Dominic na baadae kuwapa wanafunzi wa shule hizo elimu juu ya masuala ya
kifedha.
Katika
Mkoa wa Iringa, vifaa vilivyokabidhiwa kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
ni; mashuka, vitanda vya kujifungulia kwa akina mama, na vitu mbalimbali
kama pampasi, mafuta ya kujipak na sabuni kwa ajili ya watoto.
Akimkabidhi
vifaa hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Robert Salim, Mkuu wa Idara ya
Huduma kwa Wateja wa NMB - Abella Tarimo alisema, Benki ya NMB
imejiwekea utaratibu maalum wa kurejesha kwa jamii asilimia moja ya
faida wanayoipata ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa wadau wa Benki hiyo
lakini pia na wafanyakazi hua wanajipanga kwa sehemu yao na kutoa
walichonacho kwa jamii.
Akipokea
msaada huo Mganga Mkuu wa Mkoa alishukuru Benki hiyo kwa msaada huo
akieleza kuwa umefika wakati muafaka kwani kumekuwa upungufu wa baadhi
ya vifaa kulingana na idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa hospitalini hapo
kutoka ndani na nje ya mkoa.
Dkt.
Salim alisema kuwa hospitali hiyo inategemewa na mkoa mzima na mkoa wa
jirani hivyo upungufu wa vifaa hivyo upo kwani wagonjwa ni wengi lakini
kuna upungufu wa vitanda, mashuka na vitendea kazi hivyo kitendo cha NMB
kuleta baadhi ya vifaa hivyo imefanikiwa kutatua changamoto hizo.
Katika
Mkoa wa Kagera, Benki hiyo imekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi
milioni tano katika kituo cha Afya Rubale - Wilaya ya Bukoba Vijijini,
ambapo vifaa vilivyotolewa ni vitanda sita na magodoro yake pamoja na
mashuka.
Akikabidhi
vifaa hivyo Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Ziwa Baraka Ladislaus,
alisema kuwa NMB imechangia vifaa vya shilingi milioni 25 tangu mwezi
Januari mwaka huu kwa ajili ya kuboresha huduma za afya Mkoani Kagera
kama sehemu ya jitihada za benki hiyo kuunga mkono hatua za Serikali za
kuboresha sekta ya afya nchini.
No comments :
Post a Comment