Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Amina Lumuli
akizungumza na wadau mbalimbali kuhusiana na mpango wa shirika hilo
kuboresha maisha wananchi waliothiriwa na ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR)
katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja
Uhusiano wa TRC Jamila Mbarouk akitoa maelezo katika mkutano wadau
kuhusiana na mpango wa kuboresha maisha kwa wananchi walioathiriwa na
ujenzi wa Reli ya Kisasa.
Mkurugenzi
wa Huduma ya Simu kwa Mtoto wa Shirika la C-Cema Michael Marwa
akizungumza namna shirika hilo linavyofanya kazi katika masuala ya
ukatili kwa watoto.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa wa SIDO Stephen Bondo
akitoa uzoefu wa SIDO katika utoaji wa elimu ya ujasiriamali na namna
watavyoshiriki kwa wananchi katika mpango wa TRC.
Wadau
wakifatilia hotuba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC Katika ulioandaliwa
kuhusiana na mpango kuboresha maisha kwa wananchi walioathiriwa na mradi
wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TRC Amina Lumuli (katikati) wakisaini makubaliano
na Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Profesa Sylivester Mpanduji wa tatu kutoka
kushoto makubaliano hayo yamefanyika katika mkutano wa wadau uliondaliwa
na TRC.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC Amina Lumuli akibadilishana hati na mkurugenzi Mkuu wa SIDO Profesa Sylivester Mpanduji.
*Yashirikisha wadau mbalimbali wa kutekeleza mpango huo.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
SHIRIKA
la Reli Tanzania (TRC) limekutana na wadau kutoka Taasisi za Serikali
pamoja mashirika yasiyo ya kiserikali katika kuweza kushirikiana na
katika utoaji wa elimu kwa wananchi waliothiriwa na mradi wa ujenzi wa
Reli ya Kisasa (SGR) katika mpango wa kuboresha maisha.
Shirika
hilo limeandaa mpango ya kusaidia wananchi walipitiwa na mradi huo
kwani kuna wengine wametwaliwa ardhi yao kwa kuondoka katika maeneo yao
huku wengine biashara hivyo kunahitajika kuwajenga katika kurudi katika
maisha walioyazoea.
Akizungumza
na wadau hao Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Amina Lumuli
amesema mpango huo ni pamoja na kuanzisha shughuli za ujasiriamali
itakayofanywa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) pamoja na
Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) kutoa elimu kwa wananchi
waliopitiwa na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge.
Lumuli
amesema kuwa katika ujenzi huo kuanzisha mpango huo ni kutaka wananchi
hao kuona huo mradi haujaathiri maisha yao kutokana na kuwepo kwa
mpango ni kuhakikisha wananchi walioko kandokando ya reli wananufaika
na fursa mbalimbali.
Amesema
moja ya jitihada ambazo zimefanyika ni pamoja na kulipa fidia kwa wale
waliotwaliwa ardhi,nyumba yao katika ujenzi wa reli ya kisasa kwa
kuzinagatia viwango vilivyowekwa kamataifa.
Lumuli
amesema wadau hao watatumika katika maeneo mbalimbali ikiwemo kutoa
elimu kwa wananchi kwa kutumia utaalam wao wa kufanya waelewe malengo ya
serikali kujenga reli ya kisasa ambayo ni ya watanzania
Mkutano
huo ulikwenda sambasamba na kusaini makubaliano ya utekelezaji wa
mpango huo kwa baadhi ya wadau ikiwa na lengo wadau wanawafikia
wananchi walioathiriwa na ujenzi wa reli ya kisasa.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa wa SIDO Stephen Bondo
amesema kuwa SIDO imekuwa ikitoa mafunzo kwa kwa wajasiriamali na
kumekuwa na mafanikio hivyo hata hao walipitiwa na mradi wa reli ya
kisasa watanufaika.
Mkurugenzi
wa Huduma ya Simu kwa Mtoto wa Shirika la C-Sema Michael Marwa
amesema kuwa katika ujenzi huo ni kuangalia masuala ya ukatili wa kwa
watoto ikiwa ni pamoja na kutoa elimu katika eneo hilo.
No comments :
Post a Comment