Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa
Nangulukulu mkoani Lindi kuhusu ubovu wa barabara ya kutokea Lindi-
Somanga wakati alipokuwa akitokea Msibani Masasi mkoani Mwara leo tarehe
30 Julai 2020.Wananchi
wa Nangulukulu wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza nao
wakati akitokea Masasi leo
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli ukipita katika barabara ya Nangulukulu-hadi Somanga
mkoani Lindi ambapo sehemu ya barabara yake imeharibika vibaya na
kuhitaji matengenezo makubwa .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa na zawadi yake ya Jogoo alilopewa na Shaweji Mohamed
Kimbwembwe mkazi wa Somanga mkoani Lindi ambaye alifurahishwa na
utendaji kazi wa Mhe. Rais Magufuli wa kuwaletea maendeleo Wananchi
wanyonge.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Somanga Rehema
Mikidadi Ngenje Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa Shule hiyo
ya Msingi ya Somanga. Katika fedha hizo pia Rais aliagiza mwanafunzi
huyo apewe Shilingi laki moja kutoka kwenye fedha hizo mara baada ya
kuibua kero ya Shule hiyo.Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwapungia mkono Wananchi wa Somanga mkoani Lindi mara baada ya
kuwahutubia wakati akitokea Masasi mkoani Mtwara.
PICHA NA IKULU
No comments :
Post a Comment