
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza leo Jijini Dodma katika
sherehe za uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).
Meza kuu wakiwa wamesimama wakati
wa kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza sherehe za uzinduzi wa Jengo
la Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) leo Jijini Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT), Meja Jenerali, Charles Mbuge, akisoma taarifa fupi ya mradi wa
ujenzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) leo Jijini Dodoma
wakati wa uzinduzi wa jengo hilo..
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama
akisalimia katika sherehe za Uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) leo Jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Jaji Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage akitoa neno katika
sherehe za Uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Baadhi ya Viongozi wa vyama vya
siasa nchini waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa Jengo la Tume
ya Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dodoma.

Baadhi ya viongozi wa vyombo vya
ulinzi na usalama wakifatilia sherehe za Uzinduzi wa Jengo la Tume ya
Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dodoma.
PICHA NA ALEX SONNA
………………………………………
Na.Majid Abdulkarim, Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ametoa siku 14 kwa taasisi na
mashirika yanayodaiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA GUARD) kuwa
wamelipa madeni hayo ili kuliwezesha jeshi hilo kutekeleza miradi
kikamilifu.
Agizo hilo amelitoa leo Jijini Dodma katika sherehe za uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa
kila taasisi iwe ya serikali au binafs ndani ya siku 14 kila tasisi kuwa
imelipa deni lake na kupewa listi kuwa wamelipa na JKT.
Rais Magufuli ametoa wito kwa
viongozi wa siasa nchini kuendesha kameni zao kwa ustarabu, kunadi sera
zao bila kutoa kauli chafu na kutanguliza uzalendo kwa kulinda amani na
kuufanya uchaguzi wa mwaka huu kuwa maalumu.
“Katika siasa zetu tujitahidi
kunadi sera zetu kwa kumtanguliza mungu lakini pia tujenge hoja wakati
wa kuwasilisha sera zetu kwa wananchi ili kuweza kuwapa nafasi wananchi
kujua yupi kiongozi sahihi anawafaa pale itakapo fika 28 Oktoba, 2020
siku ya Uchaguzi Mkuu.
Katika hatua nyingine Rais
Magufuli ameiongezea Tume ya Taifa ya Uchaguzi Milioni 500 kwa ajili ya
kukamilisha vifaa muhimu vinavyotakiwa katika jingo hilo ili kuweza
kutekeleza shughuli zake ipasavyo.
“Lakini pia vifaa vilivyopo katika
ofisi zilizokuwa Dar es Salaam pia mviamishie huku ili kuweza
kurahisisha sghuli zenu na kuleta ufanisi mzuri katika utendaji kazi
wenu” amesisitiza Rais Magufuli.
No comments :
Post a Comment