Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga akikagua bidhaa zinazozalishwa na Bodi ya
Nafaka na Mazao Mchanganyiko wakati alipotembelea na kukagua ufanisi wa
kinu cha kukoboa nafaka wakati akiwa katika ziara ya kikazi Jijini
Arusha hivi karibuni.
Muonekano wa vihenge vya
kuhifadhia nafaka vya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Jijini Arusha
pamoja na baadhi ya ofisi zikiwa katika uchakavu
Waziri wa Kilimo Japhet
Hasunga akizungumza na Meneja wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko
Kanda ya Arusha Ndg Idd Mkomalasa wakati alipotembelea kukagua bidhaa
zinazozalishwa na Bodi hiyo akiwa katika ziara ya kikazi Jijini Arusha
hivi karibuni.
Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga akiongozana na Meneja wa Bodi ya Nafaka na
Mazao Mchanganyiko Kanda ya Arusha Ndg Idd Mkomalasa wakati
alipotembelea CPB kukagua bidhaa zinazozalishwa na Bodi ya Nafaka na
Mazao Mchanganyiko wakati alipotembelea na kukagua ufanisi wa kinu cha
kukoboa nafaka wakati akiwa katika ziara ya kikazi Jijini Arusha hivi
karibuni.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha
Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga ametoa siku 14 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya
Nafaka na Mazao mchanganyiko Dkt Anslem Moshi kukamilisha malipo ya
wakulima wote waliouza korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Waziri
Hasunga ametoa agizo hilo wakati alipotembelea na kukagua shughuli za
utendaji kazi zinazofanywa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko
Jijini Arusha.
Amesema
kuwa Bodi hiyo ilipewa dhamana la kununua korosho mwaka 2018 kwa niaba
ya serikali na tayari serikali imeshatoa fedha zote kwa ajili ya
wakulima lakini bado CPB haijakamilisha malipo hivyo ni lazima malipo
yakamilike ndani ya siku hizo.
“Ndani
ya siku 14 sitaki kusikia malalamiko ya wakulima lazima wakulima wote
wawe wamelipwa fedha zao haraka iwezekanavyo” Alisisitiza
Katika
ziara hiyo pia Waziri Hasunga amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya
Nafaka na mazao mchanganyiko kuwasilisha haraka mpango kazi wa namna
viwanda hivyo vitakavyofanya kazi kwa ajili ya kutengeneza bidhaa
zitakazohitajika na wateja na kukidhi matarajio ya serikali ikiwa ni
pamoja na kuainisha idadi ya watumishi wanaohitajika.
Hasunga
ameiagiza kampuni ya Monaban ambayo ilikuwa imekodisha kiwanda hicho
kutekeleza maagizo ya serikali yaliyotolewa mwaka jana ya kuhamisha mali
zao zote zilizopo katika eneo hilo la serikali kwani kesi mahakamani na
notisi ilishaisha.
Akiwa
kiwandani hapo Waziri Hasunga amebaini uchakavu wa mitambo iliyopo
pamoja na uchache wa watumishi wanaofanya kazi katika kiwanda hicho
hivyo ameagiza kufanyika ukarabati wa majengo hayo kuanzia mwezi Agosti
badala ya Octoba kwa taasisi hiyo ilivyopanga.
“Tukisubiri
mpaka mwezi wa kumi tutakuwa tumechelewa kwa kuwa mvua zitaanza
kunyesha jambo ambalo litapelekea kushindikana kufanyika ukarabati”
Amesema
Amesema
kuwa Lengo la serikali ni kufufua viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani
ya mazao ya nafaka nchini ili kuzalisha bidhaa mbalimbali kama unga N,k
na kuuza katika masoko ya ushindani ndani na nje ya nchi.
No comments :
Post a Comment