Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi (katikati), kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nchi George
Simbachawene na mwisho kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi, Dkt.
Faraji Mnyepe wakifuatilia mkutano kwa njia ya video conference, Jijini
Dar es salaam.
Mawaziri pamoja na baadhi ya
Makatibu Wakuu/Maafisa waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano
kwa njia ya Video Conference, jijini Dar es Salaam
Mkutano ukiendelea
*********************************
Mkutano wa
Mawaziri wa Kamati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya
Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa ngazi ya Mawaziri
umefanyika kwa njia ya
Mtandao (Video Conferencing) na kujadili masuala
ya Siasa, Ulinzi na Usalama.
Mkutano huo
umefanyika chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya
Kimataifa wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Sibusiso Busi Moyo na
utakutanisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mambo ya Ndani, Ulinzi pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi
na Usalama kutoka nchi wanachama wa SADC. Ujumbe wa Tanzania umeongozwa
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi.
Mkutano huo
umehudhuriwa na nchi 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Afrika
Kusini, Botswana, Comoro, DRC, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius,
Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe
na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments :
Post a Comment