Friday, June 26, 2020

BARAZA LA VETERINARI TANZANIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFUGAJI NCHINI

0

Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania Dkt.Bedan Masuruli,akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa juu ya Afya ya Mifugo nchini pamoja na kuwataka madaktari kuhuisha majina yao kwenye daftari la usajili wa madaktari.
……………………………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
Baraza la Veterinari  nchini limeweka mpango mkakati juu ya kutatu changamoto za wafugaji ili kuongeza uzalishaji na kuleta tija katika sekta ya ufugaji nchini.
Kauli hiyo imetolewa  leo na  Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania Dkt.Bedan Masuruli, wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma juu ya kuboresha huduma za ufugaji nchini.
Aidha Dkt.Masuruli amesema kuwa wamejipanga kusambaza wataalamu wa mifungo ngazi za msingi ili kuwa karibu na wananchi na kuwashauri namna ya kuipatia kinga mifugo hiyo na kuleta tija katika ufugaji wao.
Dkt.Masuruli amesema kuwa ili kufikia adhima hiyo amesema kuwa lazima wataalamu wote wa ngazi ya msingi kusajiliwa, kujiandikisha na kujiorodhesha katika daftari ili kusaidia wizara ya mifugo  kujua ubora wa wataalamu walionao katika maeneo ya kusaidia wananchi katika kuongeza tija sekat ya ufugaji.
Aidha Dkt.Masuruli amesema kuwa wameongeza muda kwa wataalum kuhuisha majina yao kwenye daftari la usajili wa madaktari kabla ya tarehe 1 julai mwaka huu wawe tayari wamejisajili
“ Baada ya kuhuisha taarifa zao hao wataalamu watapatiwa vitambulisho maalum ili kusaidia wafugaji na wananchi kutambua kuwa ni mtaalamu aliyekidhi viwango hivyo mwananchi anaweza patiwa huduma kwa kupata ushauri, kinga na namna ya kuboresha ufugaji ili kufikia mafaniko makubwa”, Dkt.Masuruli
Dkt.Masuruli amesema kuwa Wataalamu hao katika maeneo yao watatakiwa kuwasilisha taarifa za wafugaji wizarani ili kusaidia serikali kuandaa mpango kazi wa kutatua changamoto zilizoshindikana kutatuliwa na wataalaum hao.
Hata hivyo Dkt.Masuruli amesema kuwa Lengo kuu la kusogeza huduma hizi kwa wananchi ni kutaka kuhakikisha wanapatiwa huduma bora zinazokidhi viwango na itasaidia kubaini magonjwa yanayojitokeza katika mifungo ya wanachi wanao wahudumia na kuwasaidia kwa ukaribu.
“ Natoa wito kwa vituo vyote vya afya ya wanyama kuanzia Julai Mosi Mwaka huu kuweka mpango wa muda wa miezi mitatu kupata hadubini katika vituo hivyo ili kusaidia kujua magonjwa katika mifugo ya wanachi wao wanao wahudumia”, amesema Dkt.Masuruli
Dkt.Masuruli ameongezea kuwa   wananchi kupata na kunufaika na ufugaji wanahitaji wataalamu wa mifugo kuwa karibu na wafugaji ili kuwasaidia kuwapatia huduma bora itakayokidhi viwango na kuleta tija kwa asilimia kubwa na kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

No comments :

Post a Comment