
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
(Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiangalia mafuta ya alizeti aina ya
Sunbelt yanayozalishwa katika kiwanda cha SUNSHINE kilichopo Zuzu
Mkoani Dodoma. Waziri alitembelea kiwandani hapo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
(Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiangalia na kupokea maelezo kuhusu
namna chupa, ndoo na madumu yanavyotengenezwa kwa ajili ya kuhifadhi
mafuta ya sunbelt yanayotengenezwa na kiwanda cha SUNSHINE kilichopo
Zuzu Dodoma, wa kwanza kushoto ni Afisa viwango wa kiwanda hicho
Bi.Upendo Mganda. Kulia ni Meneja Biashara na maendeleo Bw. Krishna Urs.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
(Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiangalia na kupokea maelezo kutoka
kwa Mtaalam wa viwango wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kula ya
Sunbelt Bi.Upendo Mganda kuhusu mitambo inayochakata alizeti kwa ajili
ya kuzalisha mafuta hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kiwanda
cha SUNSHINE.
……………………………………………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.
Angellah Kairuki ametoa rai kwa Watanzania kuwekeza katika sekta ya
mafuta ya kula kwa
kuzingatia uhitaji na soko lililopo ndani na nje ya
nchi.
Ametoa rai hiyo
Mei 28, 2020 alipotembelea na kukagua kiwanda cha kuzalisha mafuta ya
kula cha SUNSHINE kinachozalisha mafuta yanayotengenezwa kwa kutumia
malighafi ya alizeti yanayoitwa Sunbelt kilichopo katika eneo la Zuzu
Jijini Dodoma.
Akiwa katika
ziara hiyo, yenye lengo la kukagua, kusikiliza na kutatua changamoto za
wawekezaji nchini.Waziri Kairuki alipongeza uwekezaji katika kiwanda
hicho chenye uwezo wa kuzalisha tani 25 kwa siku na kilichowekeza zaidi
ya shilingiBilioni 230.
“Niwapongeze kwa
uwekezaji mkubwa mlioufanya katika eneo hili tangu mwaka 2015 na hii
inaleta chachu kwa wawekezaji wazawa kuona fursa na soko la malighafi
wanazozalisha hasa zao la alizeti,”alisema Waziri Kairuki
Aliongezea kuwa,
ni vyema watanzania wakaendelea kuchangamkia fursa ya kilimo cha zao la
alizeti kwa kuzingatia uhitaji mkubwa wa mafuta ya kula nchini kwani
nchi imekuwa ikipoteza zaidi ya shilingi bilioni 443 kwa mwaka kwa
kuagiza mafuta nje ya nchi.
Aidha Waziri
alibainisha kuwa uwekezaji huo ni miongoni mwa fursa muhimu na kuwataka
wenye uwezo kulima zao hilo kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo kwa vile
zao hilo linastawi katika ukanda huo.
Alitumia fursa
hiyo kuendelea kuwasihi wataalam wa masuala ya kilimo kutoa elimu kwa
umma kuhusu kilimo bora cha zao hilo ili kuwa na utaalam wa kutosha
kuhusu kilimo cha zao hilo ili kutumia mbinu za kisasa na zenye
kuzingatia viwango vinavyotakiwa.
Akitoa taarifa ya
kiwanda hicho, Meneja Biashara na Maendeleo wa kiwanda hicho Bw.
Krishna Urs alieleza changamoto wanayokabiliana nayo ni uhaba wa
malighafi kwa ajili ya uzalishaji na kuendelea kutoa wito kwa wadau
kuitumia fursa ya kilimo cha zao hilo ili kuendana na mahitaji halisi.
“Ni muhimu
kuwekeza zaidi katika alizeti kwa sababu soko lake lipo na hii itatatua
changamoto ya kuzalisha kwa uchache na kuwafikia wananchi wengi na
kuapata soko la nchi za nje”, alisema Krishna.
Naye Afisa
Viwango wa kiwanda hicho, Upendo Mganda alipongeza uwekezaji huo kwa
kuwa, umesaidia kutoa ajira na vibarua kwa wananchi walio wengi.
“Tunashukuru
uwepo wa kiwanda umetusaidia kupata ajira na wazawa wameweza kuuza
malighafi zao kiwandani hapa kwa bei yenye tija,” alisema Upendo
Aidha aliongezea
kuwa, ni kiwanda chenye tija kwa kuzingatia uwezo wake wa uzalisha tani
24 hadi 25 kwa siku na kinafanya vizuri sokoni kwa kuzingatia kuwa
mafuta yanayozalishwa hayana kemikali zenye athari kwa watumiaji.
“Uzalishaji ni wa
kuridhisha japo kuna changamoto ya uchache wa malighafi unaochangia
kusuasua kwa uzalishaji na kusababisha kuzalisha kwa msimu si ya mavuno
pekee inayochangia kutolifikia mahitaji halisi nchini,”alisema Upendo.
No comments :
Post a Comment