Moja ya Shauri kiliendesha kwa njia ya Mahakama Mtandao
**************************************
Na Magreth Kinabo –Mahakama
Mahakama ya Tanzania imefanikiwa
kuendesha mashauri 4,711 kwa njia ya Mahakama Mtandao maarufu kama
‘Video Conference’ ikiwa ni hatua mojawapo za kujikinga na
maambukizi
ya Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 1 9 katika
kipindi cha miezi miwili.
Mashauri hayo yamesikilizwa kwa
njia hiyo, kufuatia utekelezaji wa agizo la Jaji Mkuu wa Tanzania,
Prof. Ibrahim Hamis Juma alilolitoa Machi 23, mwaka huu la
kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuwaepusha
Watumishi wa Mahakama, Magereza, wafungwa na mahabusu na wateja wengine
wa Mahakama dhidi ya maambukizo hayo, wakati shughuli za utoaji haki
zikiendelea kufanyika.
Agizo hilo lilitolewa na Prof. Juma kupitia mkutano wake na
waandishi wa habari uliofanyika Jijini Mwanza, la kuongeza matumizi ya
TEHAMA kwenye kipindi hichi ambacho Tanzania na dunia kwa ujumla
kukumbwa na janga la ugonjwa huo.
Akizungumzia kuhusu usikilizaji wa
mashauri kwa kutumia teknolojia hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Bw. Machumu Essaba alisema
imelipunguzia pia Jeshi la Magereza gharama za usafiri wa kila siku za
kuwaleta wafungwa au mahabusu mahakamani na msongamano.
‘‘Njia hii imetumika katika
kipindi cha ugonjwa huu, kuanzia Machi 23, mwaka huu hadi Mei 26, mwaka
huu, ambapo Mahakama ya Rufani Tanzania, imesikiliza mashauri 48
kupitia vikao vitano, kati ya hivyo vitatu vilifanyika katika Jiji la
Dar es Salaam, vilivyohusisha mashauri 30 na kimoja Tabora
kilichohusisha mashauri tisa na kingine Iringa kilichokuwa na mashauri
tisa,’’ alisema Essaba.
Alisema kuwa Mahakama Kuu ya
Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imesikiliza mashauri 3,188 kati ya
hayo, mashauri 804 ymesikilizwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Mahakama za Wilaya, Kinondoni 714, Ilala 992, Temeke 523, na Kigamboni
155.
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya
Mbeya, Mahakama ya Mkoa na Wilaya mashauri yaliyosikilizwa kwa
teknolojia hiyo ni 367, kanda zingine ni Tanga 310, Musoma 158, Tabora
130, Dodoma 78, Mtwara 66, Moshi 46, Arusha 41, Kigoma, 37, Sumbawanga
23, Iringa 15, Songea 14, Shinyanga 12, Mwanza 28 na Bukoba 5.
Essaba alifafanua kwamba Mahakama
Kuu Divisheni za Biashara imesikiliza mashauri 55 na Kazi mashauri 90,
ambazo zilitumia vifaa vilivyopo kwenye maeneo yao.
Aidha aliongeza kwamba zaidi
mashauri 300 yamesikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza
kwa kutumia simu ya mezani ‘Teleconference’ kwa sababu kuna tatizo la
ukosefu wa huduma ya mtandao ‘internet’ kwenye ofisi za
Mwanasheria wa Serikali, hali inayosababisha kutumia njia hiyo.
Uongozi wa Mahakama katika kuunga
mkono juhudi za Serikali za kukabiliana na Virusi vya Corona ulikabidhi
vifaa vya TEHAMA kwa Maafisa TEHAMA wa kanda 16 za Mahakama Kuu
yaTanzania Aprili 16 mwaka huu ili kuziwezesha Mahakama nyingine
kusikiliza mashauri kwa teknolojia hiyo,
Awali teknolijia hiyo ilikuwa
inatumika katika vituo sita, ambavyo ni mfumo huo, umefungwa ambavyo
ni Mahakama Kuu ya Tanzania katika Kanda za Dar es salaam, Mbeya, na
Bukoba pamoja na Kituo cha Mafunzo cha Kisutu, Gereza la Keko na Chuo
cha Uongozi wa Mahakama (IJA), Lushoto.
No comments :
Post a Comment