Monday, March 2, 2020

Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC Kufanyika tarehe 16 – 17 Machi



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiriikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo ktk picha) kuhusu Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC
utakaofanyika tarehe 11 – 17 Machi, 2020 Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiriikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakaofanyika tarehe 11 –
17 Machi, 2020 Jijini Dar es Salaam.
***************************
Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unatarajiwa kufanyika hapa nchini kuanzia tarehe 11 hadi 17 Machi, 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushiriikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa mkutano huo utafanyika kuanzia tarehe 12 hadi 17
Machi 2020 ambapo utatanguliwa na mkutano wa wataalamu pamoja na Makatibu Wakuu na kufuatiwa na mkutano wa mawaziri tarehe 16 – 17 Machi, 2020.

“Pamoja na mambo mengine, mkutano huu utahusisha Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mawaziri wa Fedha, Uchumi na Mipango pamoja na Mawaziri wa Viwanda na Biashara,”Amesema Prof. Kabudi.

Waziri Kabudi amesema kuwa mkutano huo utahudhuriwa na Mawaziri 16 kutoka Nchi wanachama wa SADC za Angola, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Comoro, Lesotho, Mauritius, Madagascar, Kongo DRC, Shelisheli, Msumbiji,
Afrika Kusini, Tanzania, Malawi, Botswana pamoja na Eswatini).

Aidha, Kwa mujibu wa Mhe. Waziri Kabudi, Mkutano huo utakuwa mkutano wa kwanzawa SADC wa Baraza la Mawaziri kuendeshwa kwa lugha ya Kiswahili baada ya lugha hiyo kuwa miongoni mwa lugha rasmi za Jumuiya
hiyo.

Prof. Kabudi aliongeza kuwa, mkutano huo utajadili masuala mbalimbali muhimu kwa mustakabali wa maendeleo na ustawi wa nchi wananchama wa SADC.

“Mktano huu utapokea taarifa na kutolea maelekezo taarifa za vikao mbalimbali vya kisekta vya kamati za mawaziri ambavyo vimefanyika nchini tangu Septemba 2019,” Ameongeza Prof. Kabudi.

No comments :

Post a Comment