Waziri wa Nishati Dkt.Medard
Kalemani akitoa maelekezo kwa mameneja pamoja na wakandarasi kuondoa
nguzo za umem zilizolazwa ovyo barabarani akiwa njiani kwenda kuwasha
umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Waziri wa Nishati Dkt.Medard
Kalemani,akisalimiana na viongozi mara baada ya kuwasili katika kata ya
Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma kwa ajili ya kuwasha umeme.
Mkuu wa wilaya ya Chemba Simon
Odunga,akizungumza kabla ya Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani,kabla
ya kuwasha umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Mbunge wa Chemba, Juma
Nkamia,akizungumza na wananchi kabla ya Waziri wa Nishati Dkt.Medard
Kalemani,kabla ya kuwasha umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba
mkoani Dodoma.
Waziri wa Nishati Dkt.Medard
Kalemani,akizungumza na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa
kuwasha umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Sehemu ya wananchi wakifatilia
hotuba ya Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani,alipokuwa akizungumza
nao kabla ya kuwasha umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani
Dodoma.
Waziri wa Nishati Dkt.Medard
Kalemani,akikata utepe kuashiria uwashaji wa umeme katika kata ya Farkwa
wilayani Chemba mkoani Dodoma.
………………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Chemba
Waziri wa Nishati Dkt.Medard
Kalemani amewaonya wakandarasi nchi nzima wanaotelekeza miradi ya...
umeme
vijijini (REA) kuacha mara moja tabia ya kulaza ovyo nguzo za umeme
barabarani huku zikikaa muda mrefu bila kusimikwa.
Waziri Kalemani ametoa onyo hilo wakati akiwasha umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Akiwasha umeme kwenye
kata hiyo, Waziri Kalemani ameshuhudia kuzagaa kwa nguzo barabarani
jambo lililomkera na kuagiza wakandarasi hao kuacha tabia hiyo.
“Kuna shida moja
naomba nitoe onyo la mwisho nimepita barabarani nguzo zimelala, Meneja
wa Kanda na Mkoa simamia haya nimetoa siku tatu kwa nguzo zote
zilizolala kwenye mkoa wote wa Dodoma ziondolewe zikajengwe tofauti na
hivyo Mhandisi uache kazi na wewe mkandarasi tutakuandikia barua ya
kusitisha mkataba wako,”amesisitiza.
Aidha, amemtaka
Meneja wa Mkoa wa Dodoma kusimamia suala hilo na kumtaka kumwandikia
barua mkandarasi atakayeshindwa atakayeacha nguzo hizo zikikaa muda
mrefu na kuoza.
“Hatuwezi kuacha
fedha ya serikali ikichezewa kwa kuacha nguzo ziendelee kuoza, hili ni
onyo la mwisho na ni onyo kwa wakandarasi wote nchi nzima ni marufuku
nguzo kulazwa chini zikifika ndani ya siku tatu zikasimikwe wananchi
wapate umeme,”ameonya.
Kwa upande wake,
Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia amesema umeme huo utasaidia kubadilisha
maisha yao ya kila siku kwa kufanya biashara za kujiongezea kipato.
Naye, Mkuu wa wilaya
ya Chemba Simon Odunga, ameishukuru serikali kwa kupeleka umeme kwenye
eneo hilo na kwamba kumechangia kuongeza maendeleo katika eneo hilo.
No comments :
Post a Comment