Mkurugenzi
wa Mashtaka nchini (DPP), Bw. Biswalo Mganga (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na maofisa wa Mahakama na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi (kushoto kwake) baada ya kuzindua Jukwaa la Haki Jinai hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Bw. Biswalo Mganga (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, baada ya kuzindua Jukwaa la Haki Jinai hivi karibuni.
Na Ismail Luhamba, Singida
AKIWA
kwenye ziara ya kikazi mkoani Singida Mkurugenzi wa Mashtaka nchini
(DPP), Bw. Biswalo Mganga amewataka wakuu wa mikoa nchini kote
kufanya uzinduzi rasimi wa majukwa ya haki jinai katika mikoa yao
ilikuyapa nguvu majukwa hayo ya kufanya kzi kwa ufanisi.
Ameyasema
hayo mkoani singida wakati wa hafla ya uzinduz wa Jukwaa la Haki Jinai
katika mkoa wa Singida hafla iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa
mkoani hapa jana.
Akifafanua
kuhusu majukwaa ya haki jinai Mganga amesema lengo ni kuhakikisha
shughuli za kijinai ndani ya mkoa zinakwenda vizuri
Amesema
azma yake hasa ni kuweka stratejia, kuratibu, kubuni na kuhakikisha
mwenendo mzima wa makosa ya kijinai yanaratibiwa kwa ufanisi mkubwa
“Mathalani
changamoto kama mlundikano wa mahabusu kwenye vizuizi vya polisi au
magerezani ni mojawapo ya jukumu la jukwaa hili katika ufuatiliaji wa
karibu zaidi,”
Aidha,
Mganga ameongeza kuwa majukwaa haya kwa mujibu wa sheria yana haki ya
kuleta mapendekezo katika ofisi ya taifa ya mashtaka yanapoona inafaa
hususan kwenye eneo la mabadiliko yoyote yanayoweza kuleta tija
kulingana na jiografia ya sehemu husika
Sambamba
na hilo, akiwa ziarani mkoani hapa amefuta kesi 85 zinazohusiana na
rushwa na udanganyifu ndani ya gereza la Manyoni, ikiwa ni mwendelezo wa
juhudi za serikali katika kupunguza mlundikano wa mahabusu magerezani
“Kuanzia
majira saa 5 asubuhi jana mpaka saa 12 jioni nilipata nafasi ya
kusikiliza baadhi ya mahabusu wa gereza la manyoni na mwisho kwa wale
waliokiri kuwa wamefanya makosa hayo na hawatarudia tena nikaamua kufuta
kesi hizo zipatazo themanini na tano,” amesema Mganga
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amesema uwepo
wa Jukwaa la haki jinai ngazi ya mkoa ni kuongeza usalama na amani
ndani ya mkoa husika
Amewataka
wajumbe wa jukwaa hilo kufanya kazi kwa umoja na uzalendo wa hali ya
juu ili kuhakikisha uhalifu na viashiria vyake ndani ya mkoa vinapungua
na kufutika kabisa
“Tafsiri
ya Jukwaa hili ni ile ile azma ya Mheshimiwa Rais ya kuendelea
kuwajali, kuwathamini na kuwapenda wananchi wake, kwa maana ya chachu na
njia ya kutuepusha na uhalifu,” amesema Nchimbi
Akitoa
neno la shukrani, Mwenyekiti Mteule wa Jukwaa la Haki Jinai mkoani
hapa, Rose Chilongozi alisema chombo hicho kitaangalia namna ya kujikita
katika kutoa elimu kwenye Nyanja mbalimbali
“Ni
ushirikiano pekee kwa kila mtu kwa nafasi yake ndio utakaotuwezesha
kukabiliana kikamilifu na uhalifu…ni fursa ya wateuliwa kukaa pamoja kwa
umoja na kutafakari na kuweka mikakati,” amesema Chilongozi
Mmoja
wa wajumbe wa Jukwaa hilo, ambaye ni Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa
Singida, Safina Muhindi amesema chombo hicho kinakwenda kurahisisha na
kuwezesha ushahidi kupatikana kwa urahisi na uendeshaji wa mashauri ya
kijinai kuwa wa haraka zaidi,” amesema Muhindi
No comments :
Post a Comment