
*********************************
EMMANUEL MBATILO
Shirika la Uwakala wa Meli
Tanzania (TASAC) limewahikikishia mawakala binafsi wa meli kuwa
litafanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria iliyopo na halitaingilia
shughuli
zinazopaswa kufanywa na watu binafsi kama wengine wanavyodhania
na kulalamikia uwepo wake.
Akizungumza na waandishi wa habari
mkurugenzi mkuu wa (TASAC) Mhandisi EMMANUEL NDOMBA amesema kuwa TASAC
imeundwa kwa mujibu wa sheria na haijawekwa kwaajili ya kufuta mawakala
wengine bali ni kusimamamia shughuli za meli kwa uhakiki na usalama
zaidi.
Ameongeza kuwa mpaka kufikia
February 17 mwaka huu TASAC itakuwa imeshaanza kushughulikia kazi zote
nne walizopewa kwa mujibu wa sheria ambapo watakuwa wanashughulikia meli
zote za kijeshi,meli za mafuta, ikiwa ni pamoja na kushughulikia mizigo
inayoingizwa na kusafirishwa na jeshi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
udhibiti usafi wa majini DEOGRATIAS MKASSA amesema kuwa hivi sasa wapo
mbioni kuweka vigezo vyenye tija kwa watendaji na watoa huduma wote
katika shughuli za uwakala wa meli ili kuhakikisha matuzi ya bandari
nchini yanaongezeka mara dufu.
Aidha TASAC mpaka sasa wameweza
kufuta tozo takribani saba ambazo zimekuwa sumbufu kwa wateja pia
imeweza kufanikisha kuwasilisha gawio la faida la takribani billion 10.1
kwa serikali.
No comments :
Post a Comment