
Na Emmanuel J. Shilatu
Heri ya Mwaka mpya
2020 Ndugu yangu Mtanzania. 2020 ni Mwaka mwingine wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anaendelea kuongoza.
Naam! Watanzania tumemchagua Rais Magufuli aendelee kuongoza 2020 ili
tuone kazi aliyoianza inakamilika ipasavyo na Watanzania wananufaika na
matunda ya kazi hiyo.
(i) Kuhamia Dodoma
Wazo la Serikali
kuhamia kwenye makao makuu ya nchi mkoani Dodoma liliasisiwa na Baba wa
Taifa, Mwalimu Nyerere mwaka 1973 lakini lilishindwa kutekelezwa katika
awamu zote. Si awamu ya kwanza, wala ya pili, ama ya Tatu au ya nne bali
limeweza kufanikiwa kwenye utawala wa Serikali ya awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Magufuli. Leo hii karibia Serikali yote imehamia
Dodoma. Wizara, taasisi na idara za Serikali, Waziri Mkuu wameshahamia
Dodoma mpaka Rais Magufuli naye amehamia Dodoma. Iliasisiwa na Mwalimu
Nyerere, ikahaidiwa kwenye ilani ya uchaguzi, imekuja kutekelezwa vyema
na Rais Magufuli lakini uhamiaji huu ni kwa awamu awamu. 2020 Watanzania
tumemchagua Rais Magufuli akaimalizie hii kazi iliyokwama hapo awali
bali yeye ameiweza kwa kuhakikisha Serikali kamili pamoja na idara zake
zinahamia Dodoma.
(ii) Ujenzi wa Stiegler’s Gorge ama Mto Rufiji
Utawala wa awamu ya
kwanza uliokuwa ukiongozwa na Mwalimu Nyerere ulikuja na wazo la kujenga
Stiegler’s Gorge mnamo mwaka 1981 lakini umeshindwa kufanyika mpaka
awamu hii ya 5 inayoongozwa na Rais Magufuli umeamua kufufua na
kuliendeleza wazo hili ambalo pasipo ushujaa na ujemedari wa Rais
Magufuli basi usingefanyika. Mradi wa Stiegler’s Gorge kupitia Mto
Rufiji utafanikiwa kuzalisha Megawattz 2115 hadi utakapo kamilika ambapo
utakuwa umeme mkubwa kuzidi huu unaotumika sasa. 2020 Watanzania
tumemchagua Rais Magufuli ahakikishe ukamilifu wa mradi huu ambao
utajenga uhakika wa umeme nchini, utashusha bei ya umeme nchini na pia
utasaidia kuimarisha sekta ya viwanda nchini. Ni kwa uwepo wa uongozi
imara wa Rais Magufuli pekee atasimamia vyema ukamilifu wa mradi huu
ambao ni mkombozi wa umeme mjini hadi vijijini.
Pamoja na changamoto
zote Dkt Kalemani: Hadi kufikia leo vijiji 8,818 kati ya vijijini
12,000 nchini vimepata umeme kutoka vijiji takribani 2,000 ushee tu
vilivyokuwa na umeme 2015. Mwaka 2020 tumemchagua Rais Magufuli
akamilishe kazi ya kusambaza umeme vijiji vyote nchini vilivyosalia.
(iii) Ujenzi wa reli ya kisasa (SGR)
Ni takribani miaka
120 ambapo historia iliandikwa mwaka 1912 kwa Serikali ya kikoloni
kujenga Reli inayotumia dizeli. Leo hii kwenye sekta ya reli Rais
Magufuli amefanya makubwa. Kwanza amefufua usafiri wa Dar – Moshi
uliokuwa umekufa kwa zaidi ya miaka 25; Ameimarisha usafiri wa reli wa
Dar – Dodoma – Kigoma ambapo sasa ni wa uhakika zaidi.
Tuachane na hayo,
kuna hili la ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha Standard gauge
(SGR) ambapo awamu ya kwanza imeanzia Dar – Morogoro na baadae Morogoro –
Dodoma na kumalizia Dodoma – Mwanza kukamilisha umbali wa Kilomita
1219.
2020 Watanzania
tumemchagua Rais Magufuli ahakikishe ukamilifu Reli hiyo ulete tija
kwenye usafirishaji, Kilimo, utalii, uzalishaji na kibiashara. SGR
itakuwa na uwezo wa kubeba tani milioni, 10,000, kwa mkupuo sawa na
malori 500 yenye tani 20, Treni tano zenye tani 10,000 na kuwa na kasi
kubwa ya 160km/saa, tofauti na ya sasa ambayo inakasi ya 30km/saa, kwa
Afrika itakuwa ni Reli pekee yenye uwezo mkubwa kama huo, tani Miliomi
10-17 zitasafirishwa kwa mwaka, kwa hiyo SGR ni mwamba sekta ya
usafirishaji nchini.
No comments :
Post a Comment