Waziri wa Nishati, Dkt, Medard
Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chemkeni mara baada ya
kuwasha umeme kijijini humo.

Wananchi wa kijiji cha Chemkeni wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt, Medard Kalemani alipokuwa akiwahutubia kijijini humo.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani( mwenye shati la bluu) pamoja na viongozi mbalimbali wakielekea
kuwasha umeme kwenye shule iliyopo kwenye kijiji cha Chemkeni.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria kuwasha kwa umeme katika kijiji cha Chemkeni.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani na viongozi mbalimbali wa Wilaya na Wizarani wakiwa katika
kituo cha kupoza umeme cha Uhuru.
**********************************
Hafsa Omar – Tabora
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard
Kalemani amesema Serikali itaanza kuchua hatua kwa wananchi wote ambao
hawataunganisha umeme kwenye nyumba zao, ambao wanauwezo wa
kulipia
27,000.
Ameyasema hayo, Desemba 22, 2019
katika kijiji cha Chemkeni kilichopo, kata ya Igwisi, Wilaya ya Kaliua,
Mkoani Tabora, wakati alipokuwa akifanya ukaguzi wa nyumba ambazo
hazijaunganishwa umeme kijijini humo.
Amesema, Hatua ambazo
zitachukuliwa ni pamoja na kupigwa mnada mifugo ambayo wanamiliki na
kulazimishwa kuunganishiwa umeme kwenye nyumba zao.
Alieleza kuwa Serikali inatumia
gharama kubwa kuhakikisha umeme unafika nchi nzima, kwahiyo asingependa
kuona wananchi hawatumi fursa hii ya kuweka umeme kwenye nyumba zao tena
kwa gharama nafuu.
Aidha, Dkt. Kalemani alichukizwa
na kitendo cha baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, kukataa kuweka umeme
kwenye nyumba zao kwa madai ya kwamba wanasubiri kufungua biashara
ambazo zitawalazimu kuunganisha umeme.
“Haiwezekani Serikali ilete
bilioni 36 kwenye Mkoa huu, halafu mkatae kutumia umeme lazima tuanze
kuwachukulia hatua na itafika mahala tutatumia nguvu kwa wananchi ambao
hawataki kuweka umeme na nitarudi hapa mwakani kufuatilia nyumba kwa
nyumba” alisema.
Waziri Kalemani, amewaagiza
TANESCO kuendelea kuwahamasisha wananchi kulipia huduma ya umeme ili
wananchi wapate hamasa ya kuweka umeme kwenye nyumba na taasisi za umma
ambazo zipo karibu na maeneo yao.
Katika ziara yake mkoani humo,
Waziri wa Nishati, aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kaliu Abel Busalama,
Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga na viongozi
mbalimbali wa vyama na Serikali, pia aliwasha umeme katika vijiji vya
Ilege,Chemkeni vilivyopo wilayani Kaliua na kukagua ujenzi wa kituo cha
kupoza umeme cha Uhuru kilichopo wilaya ya Urambo.
No comments :
Post a Comment