Na Mwandishi Wetu, Morogoro.
Aliyekuwa Waziri wa Fedha na
Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Morogoro Mustafa Mkulo (pichani) ameshangazwa
na baadhi ya watu kudai anataka kugombea ubunge katika jimbo la
Kilosa
huku akikanusha hana mpango wowote wa kugombea nafasi hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari
mjini Morogoro katika salamu za mwaka mpya wa 2020 ikiwa ni sehemu ya
kawaida yake kufanya hivyo kila mwisho wa mwaka, Mkulo amesema
ajabadilisha maamuzi yake ya kutogombea nafasi ya ubunge na kushangwazwa
na baadhi ya watu kudai anataka kuombea tena nafasi hiyo.
“Kuna watu wamekuwa wakidai nataka
kugombea tena ubunge Kilosa hizi ni habari za uongo sina mpango wa
kugombea ubunge sehemu yoyote ile hapa nchini “ amesema Mkulo.
Mkulo amesema bado anajivunia
katika miaka 10 ya ubunge jimbo la Kilosa kwa kutekeleza ilani ya chama
kwa kipindi hicho na Wana-Kilosa kuridhika na utendaji wake.
Aidha Waziri waziri huyo mtaafu wa Fedha amesema ataendelea kuwa mwanachama na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hata hivyo amefafanua kuwa pamoja
sio mbunge na wala hafikirii kugombea nafasi hiyo lakini ataendelea
kutoa mawazo yake kwa CCM na hata kusaidia wasiojiweza kwa niaba ya CCM
ili chama kiweze kutekeleza mipango yake ya kimaendeleo.
Katika salamu zake za mwaka 2020
Mkulo amesema anafurahishwa na utendaji kazi mzuri wa Rais wa awamu ya
tano Dkt John Pombe Magufuli na anaunga na wanaCCM wengi kutomuingilia
katika katika uchaguzi wa kipindi cha pili ya miaka mitano ijayo 2020
hadi 2025 ili aweze kutekeleza kwa ufasaha mipango ya kimaendeleo
alioicha katika awamu ya kwanza.
“Huu ni utaratibu wangu wa kila
mwaka kutoa salaumu za mwaka mpya tangu nikiwa mbunge na sasa ni wakati
wa kusema ukweli Rais Magufuri kwa miaka minne amefanya mengi mazuri
anahitaji pongezi kutoka kwa Watanzania hasa katika kupandisha uchumi na
kuboresha miundombinu ya nchi hii” amesema Mkulo.
Mustafa Mkulo ni Mbunge Mstaafu
ambaye aliongoza kwa miaka 10 katika jimbo la Kilosa ambapo pia katika
kipindi hicho alishika nafasi ya Waziri wa Fedha na kuacha kugombea
mwenyewe kwa hiari yake katika uchaguzi 2015 na nafasi yake ikachukuliwa
na Mbunge wa sasa Mbaraka Bawaziri ambapo amesema maamuzi yake ya
kuacha kugombea ni kutoa nafasi wa wanaCCM wengine kuchangia mawazo yao
katika kuliletea maendeleo jimbo la Kilosa.
No comments :
Post a Comment