Maafisa
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja
na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi wa Taasisi hiyo Robert
Mallya (aliyevaa safari suti) mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya
kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi namba
tatu.
Mkuu
wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Tulizo Shemu akiwaeleza wauguzi wa wodi namba tatu jinsi ya
kuwahudumia wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo ili waweze kujikinga
na maambukizi (infection) kwenye eneo ambalo limefanyiwa upasuaji (kidonda)
wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa
katika wodi hiyo.
Mkurugenzi
wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Robert Mallya akiwapongeza wauguzi wa wodi namba tatu kwa upendo waliokuwa nao
kwa wagonjwa wanaowahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha
utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.
Msimamizi
wa wodi namba ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Afisa
Uuguzi Anastazia Moshi akieleza namna wauguzi wa wodi hiyo wanavyofanya kazi ya
kuwahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa
wagonjwa waliolazwa katika Taasisi hiyo.
Maafisa
Uuguzi wa wodi namba wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na Mkuu wa
Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Dkt. Tulizo Shemu na Mkurugenzi wa
Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi Robert Mallya wakimkabidhi dawa zilizotolewa na
wauguzi wa wodi hiyo Mkuu wa kitengo cha Ustawi wa Jamii Asha Salum kwa ajili
ya wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kulipia gharama za matibabu wakati wa hafla
fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi
hiyo.
Mkurugenzi
wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi Robert Mallya, Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa
Huduma za Afya Dkt. Tulizo Shemu na Mkuu wa kitengo cha Ustawi wa Jamii Asha
Salum wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wakiwaongoza wauguzi wa wodi namba tatu
kukata keki ikiwa ni ishara ya kuonesha upendo kati yao na wagonjwa
wanaowahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa
waliolazwa katika wodi hiyo.
Afisa
Uuguzi wa wodi namba tatu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jumaa Omary
akimlisha keki mgonjwa aliyelazwa katika wodi hiyo ikiwa ni ishara ya
kuonesha upendo kwa wagonjwa wanaowahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha
utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.
Maafisa
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja
na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi wa Taasisi hiyo Robert
Mallya (aliyevaa safari suti) mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya
kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi namba
tatu. (PICHA NA: GENOFEVA MATEMU – JKCI)
No comments :
Post a Comment