Na Ahmed Mahmoud Arusha.
Waziri wa Mambo ya nje na
ushirikiano wa kimataifa,Paramagamba Kabudi amezitaka nchi za jumuiya ya
Afrika mashariki kuwekeza katika sekta ya miundo mbinu ili kuwa na
nishati ya
kutosha kwa ajili ya ujenzi wa viwanda .
Alisema hatua hiyo itawezesha
biashara kukua kwa nchi za jumuiya hiyo kiwemo kuongeza sayansi
,Teknolojia na ubunifu kwa Vijana wenye ujuzi wa kufanyakazi kwenye
viwanda hivyo.
Ameyasema hayo katika mkutano wa
Wafanyabiashara zaidi ya 1000 wa nchi za Afrika mashariki ulioandaliwa
na Baraza la Wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki (EABC)
unaofanyika kwa siku mbili jijini Arusha na kwenda sambamba na
maadhimisho ya miaka 20 ya jumuiya ya Afrika Mashariki.
Prof.Kabudi amesema kuwa,nchi
zilizo nyuma katika maendeleo ya viwanda zinapaswa kusaidiwa ili kupata
viwanda na kuweza kuzalisha bidhaa na kuuza kwenye soko la pamoja la
jumuiya ya Afrika Mashariki.
“lazima nchi ziwe na viwanda vya
kutosha na kufanyabiashara nzuri ,kwa sababu jumuiya ni ya watu wote na
lazima iwanufaishe wananchi wote”Amesema
Naye waziri wa viwanda na
biashara Innocent Bashungwa amesema kuwa uchumi wa nchi za jumuiya ya
Afrika Mashariki lazima ujengwe kupitia sekta binafsi za viwanda,kilimo,
Mifugo na kuimarisha miundo mbinu .
Amesema serikali ya Tanzania
inajitahidi kuweka mazingira Bora kwa wafanyabiashara ili biashara zao
zinakua na kuhakikisha wanafanyabiashara nje ya Tanzania bila kikwazo
chochote .
Waziri Bashingwa ametumia wasaa
huo kuwakaribisha wawekezaji kuja hapa nchini kuwekeza viwanda kwa ajili
ya vifungashio na kuviuza katika nchi wanachama.
Baadhi ya Wafanyabiashara
waliohudhuria mkutano huo ,Lomayan Laizer na Jiten Shah Mwanzilishi wa
kampuni ya Quickmarc wamepongeza mazingira mazuri yanayotolewa kwenye
nchi za ukanda huu na kuwataka kuangalia kwa kina na kutatua changamoto
mbalimbali ikiwemo ushuru na tozo mbalimbali
Walisema kuwa pia vikwazo katika
mipaka wakati wanaposafirisha bidhaa zao kutoka nchi moja kwenda nchi
nyingine imekuwa ni shemu ya changamoto hususani vipimo vya ubora na
kuwataka wakuu wa jumuiya hiyo kuboresha na uwezekano wa kuondoa
vikwazo hivyo ili kuwarahisishia Wafanyabiashara kufanya biashara zao
kwa urahisi zaidi.
Naye Erhard Mlyansi ambaye ni
Afisa masoko mkuu wa kampuni ya Motisun Group kutoka jijini Dar es
Saalamu inayotengeneza bidhaa mbalimbali za ujenzi na juisi ya Sayona
amelalamikia hatua ya kuigwa kwa bidhaa zao na kuuzwa katika nchi za
jumuiya ya Afrika mashariki Jambo ambalo limekuwa likiwasababishia
usumbufu kibiashara
No comments :
Post a Comment