Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Khamis Kigwangala akiwa na baadhi ya
wasanii wa muziki na filamu katika hifadhi ya Burigi Chato
WIZARA ya Maliasili na Utalii ipo katika
mchakato wa kupandikiza Wanyama zaidi wa aina mbalimbali katika hifadhi
mpya ya Taifa ya Burigi Chato wakiwemo Faru weupe ili iweze kuwa
kivutio kwa watalii mbalimbali ambao wameanza kutembelea hifadhi hiyo.
Akiongoza zoezi la utalii wa kutembea
kwa miguu akiwa amefuatana na wasanii wa muziki na filamu katika hifadhi
hiyo, mpya iliyopo katika mikoa ya Kagera na Chato Waziri wa Maliasili
na Utalii Dkt.Khamis Kigwangala amesema kwa mara ya kwanza Serikali ya
Tanzania imeamua kupandikiza Faru weupe katika hifadhi ya Burigi Chato.
Alisema utatifi bado unaendelea wa kuangalia namna ambavyo Faru hao
weupe wataweza kuishi katika hifadhi hiyo kwa sababu hawakuwahi kuwepo
kabisa hapa nchini.
Alisema ,Asili ya Faru weupe wanazaliana kwa wingi na kwa haraka hivyo
wakipandikizwa katika hifadhi hiyo watasaidia sana kukuza idadi ya Faru
weupe katika nchi na pia kuendelea kuwahifadhi kwa faida ya dunia nzima.
Pia alisema utafiti wa kupandikiza Faru weusi katika hifadhi hiyo
umekamilika na malisho yapo ya kutosha na kudai kuwa asili ya hifadhi ya
Burigi Chato ni nchi ya Faru historia inaonyesha kulikuwa na Faru
wengi.
Alisema pia wamesha peleka familia moja ya Simba kutoka hifadhi ya
Serengeti Mkoani Mara na kudai kuwa bado wapo kwenye uzio na wataachiwa
rasmi baada ya wiki mbili.
Msanii wa filamu Steven Mengele maarufu kama (Steve Nyerere) alisema
hifadhi ya Burigi Chato ilichelewa sana lakini awamu ya tano
imewekezekana chini ya msimamizi wake Khamis Kigwangala na wizara nzima
ya maliasili na utalii.
Mengele,alisema Burigi Chato ndio mbuga ya kwanza yenye Twiga warefu na weusi pia ina kila vivutio alivyowahi kuviona.
Single Mtamabile,maarufu kama (Rich )alisema kutembelea hifadhi unapata
uzoefu mkubwa sana katika mambo ya uhifadhi wa mazingira na utalii.
“Sisi wenyewe tulikuwa tunaona ni kawaida lakini tulipofika katika
hifadhi hii ya Burigi Chato tumeona na kujifunza vitu vingi katika
masuala ya Utalii”,alisema Mtambalike.
No comments :
Post a Comment