Naibu
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), ashiriki
Mkutano wa Masuala ya Amani, Usalama na Maendeleo ya Watu unaoendelea
katika Jiji la Niamey nchini Niger. Mkutano huo wa siku tatu ambao
umeandaliwa na Shirika la Universal Peace Federation, umewaleta pamoja
Wakuu wa Nchi na Serikali, Maspika, Manaibu Spika, Mawaziri, Wabunge,
Viongozi wa Dini na Kimila pamoja na Wakuu wa Taasisi za Kibiashara wa
Bara la Afrika kubaini na kujadili changamoto zinazosababisha uvunjifu
wa amani na usalama katika kuwaletea maendeleo Waafrika. Katika Mkutano
huo Naibu Spika ameambatana na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Zainabu
Katimba.
Pages
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment