***********************************
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amezindua chumba cha
kuhifadhia majokofu yanayotumia umeme wa jua kwenye zahanati ya
Nyakasungwa iliyopo halmashauli ya Buchosa wilayani Sengerema.
Halmashauri ya buchosa imepata
majokofu 17 kutoka Wizara ya afya mwezi oktoba 2019 kwa awamu ya kwanza
na tayari yamesambazwa kwenye na kufungwa kwenye vituo vya kutolea
huduma za afya.
Hali ya chanjo kwa halmashauri hiyo kwa kwa mwaka huu ni
asilimia 94 kutoka asilimia 79 mwaka jana na katika kampeni ya kitaifa
ya chanjo ya surua na rubella mwezi oktoba mwaka huu imefanikiwa kwa
asilimia 106.
Majokofu hayo yatasaidia
kuimarisha mnyororo baridi na hivuo kuongeza ubora na utunzaji wa chanjo
katika vituo vya kutolea huduma za afya ambayo itapelekea watoto kupata
chanjo zenye ubora kama ilivyokusudiwa
No comments :
Post a Comment