Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba ( TMDA),Gaudensia
Simwanza akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa Mawaziri
wa Afya wa nchi za SADC unaofanyika kwenye ukumbi wa BoT jijini Dar es
salaam katikati ni Bw.Christopher Migoha Ofisa Udhibiti wa Dawa Mamlaka
ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kutoka kituo cha Uwekezaji (TIC).
…………………………………….
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba
TMDA imekuwa ikitoa msaada wa kiufundi na mafunzo kwa wakaguzi wa dawa
wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za (SADC) ili nchi hizo
kwa pamoja ziweze kufikia viwango vya kimataifa katika ukaguzi na
mifumo ya udhibiti na ukaguzi wa dawa hivyo kufikia lengo la nchi zote
za SADC kudhibiti dawa kwa mifumo iliyosawa katika kuwalinda watumiaji
wa dawa na vifaa tiba.
Akizungumza na waandishi wa
habari kwenye banda la maonesho la taasisi hiyo kando ya mkutano wa
Mawaziri wa Afya na UKIMWI wa nchi za SADC, Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Mamlaka hiyo Bi. Gaudensia Simwanza amesema wakaguzi wa dawa
kutoka nchi za SADC, walio wengi wamekuja kujifunza na kupata ujuzi
kutoka (TMDA) ili kujua namna mifumo yao inavyoweza kudhibiti, ubora na
usalama wa dawa ikiwa ni pamoja na ukaguzi katika nchi zao.
Ameongeza kuwa Tanzania imekuwa
ni nchi ya kwanza Afrika kwa mifumo yake kutambuliwa na Shirika la Afya
Duniani (WHO) kwa kufikia ngazi ya tatu katika udhibiti, ubora na
usalama wa dawa (WHO Maturity Lever III).
Nchi za SADC zinafaidika na
Tanzania kwa kufikia viwango hivyo vya kimataifa kwani kwa sasa tayari
TMDA inatoa msaada wa kiufundi kwa wataalam mbaimbali na wakaguzi wa
nchi za SDAC na kutoa ushauri kwa viwanda vya kuzalisha dawa
vinavyojengwa ili kuzalisha dawa zenye viwango, Ubora na Usalama kwa
watumiaji wa dawa hizo
“Hii ni hatua ya kujivunia kama
nchi kwa kufikia viwango hivyo vya kimataifa kwa sababu hii inawafanya
watanzania pia kuwa na uhakika wa viwango vya dawa wanazotumia kwa kuwa
zimepitia katika mifumo ya udhibiti na usalama wa ubora wenye uhakika na
wa kimataifa”.
Amesema Mkutano huo wa Mawaziri
wa Afya wa nchi za SADC utajadili mambo mbalimbali kuhusu masuala ya
Afya ukiwemo UKIMWI kwa sababu hizi dawa za kufubaza UKIMWI pia ni
muhimu zipitie katika mifumo bora kabisa ya udhibiti wa ubora na usalama
ili wakati watumiaji watakapozitumia suala zima la usalama wao liwe la
kwanza kuzingatiwa.
“Ndiyo maana na sisi kama Mamlaka
ya Dawa na Vifaa Tiba tuko hapa ili kujua nini kinajadiliwa ambacho
kitafaa kwetu kuchukua hatua na kukifanyia kazi kwa upande wetu”
ameongeza Simwanza.
Ameongeza kuwa mkutano
uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu sambamba na mkutano wa nchi za
Jumuiya ya Kiuchumi ya SADC ulikuwa na lengo la kutoa mafunzo kwa
wakaguzi kutoka nchi mbalimbali za SADC namna ya kufanya ukaguzi na
udhibiti wa dawa katika viwanda vinavyozalisha dawa ili kuwa na dawa
zitakazokuwa na ubora na usalama kwa watumiaji.
Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba ( TMDA),Gaudensia
Simwanza akijadiliana jambo na Bw.Christopher Migoha Ofisa Udhibiti wa
Dawa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kutoka kituo cha Uwekezaji
(TIC). kushoto ni Mwandishi wa habari wa Chanel Ten Bi. Dorcas Raymos
Mtenga.
Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba ( TMDA),Gaudensia
Simwanza akijadiliana jambo na Bw.Christopher Migoha Ofisa Udhibiti wa
Dawa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kutoka kituo cha Uwekezaji
(TIC).
Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba ( TMDA),Gaudensia
Simwanza akimuonesha kipeperushi Bw.Christopher Migoha Ofisa Udhibiti
wa Dawa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kutoka kituo cha Uwekezaji
(TIC).
No comments :
Post a Comment