Mhandisi
wa maji kutoka shirika la Water Mission Tanzania, OpitaTarcicous
(kushoto) akitoa maelezo kwa ujumbe wa Balozi wa Denmark nchini Mette
Nørgaard Dissing-Spandet (katikati) wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji
salama katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma mwishoni mwa
wiki ambao umetekelezwa na water Mission Tanzania , Poul Due Jensen
Foundation, na wadau wengine.
Wakurugenzi kutoka taasisi za water Mission Tanzania , Poul Due Jensen Foundation wakitembelea mind main ya mradi.
Ujumbe
wa Balozi wa Denmark nchini na Wakurugenzi wa mashirika ya water
Mission Tanzania , Poul Due Jensen Foundation na Water Mission
International ukikaribishwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji
wa Nyarugusu.
Na Mwandishi WEtu.
Shirika la kimataifa lisilo la Kiserikali la Water Mission Tanzania,
linaendelea kuwanufaisha watu kwenye maeneo yenye shida ya maji nchini
kwa kutekeleza miradi ya kuwapatia maji salama ikiwemo maeneo ya kambi
ya Nyarugusu, mkoani Kigoma.
Water Mission Tanzania, imekuwa ikitekeleza miradi yake kwa kushirikiana
na taasisi za Poul Due Jensen Foundation, Grundfos Corporation, UNHCR,
Wizara ya Maji na Wizara ya Mambo ya Ndani, kuhakikisha kambi za
wakimbizi Tanzania zinakuwa na uhakika wa kupata maji salama.
Mbali na miradi ya maji kwenye kambi za wakimbizi mkoani Kigoma,
Tanzania, Water mission Tanzania, imetekeleza miradi ya maji ipatayo 24
katika maeneo mbalimbali ya vijijini nchini yenye changamoto ya kupata
maji safi, tangu ilipoanza kutoa huduma zake nchini mnamo mwaka 2014.
Hadi leo hii, wenyeji 30,000 wa Zeze, Kasanda, Kakonko, Heru Ushingo,
Mvugwe na Kazilamihunda-Juhudi wanapata maji safi na salama. Katika siku
zijazo, Water Mission Tanzania na washirika wake wanatumai kuwahudumia
hadi watu 80,000 katika jamii zinazozunguka kambi nchini Tanzania kwa
kujenga miradi ya maji safi na salama.
Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji wenye uwezo wa KW
100 kupitia nguvu ya jua katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani
Kigoma, Balozi wa Denmark nchini, Mette Nørgaard Dissing-Spandet,
amepongeza mpango huu wa ushirikiano wa mashirika yasiyo ya serikali na
Serikali katika kukabiliana na changamoto katika jamii kama kufanikisha
miradi ya kusaidia jamii kama miradi ya maji .
Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya The Grundfos Foundation (Poul Due Jensen
Foundation), Kim Nøhr Skibsted amesema, ”Mradi huu ulianza kufanyiwa
kazi mwaka 2016 wakati taasisi za Grundfos Foundation na Water Mission
zilipodhamiria kuondoa miundo mbinu ya mradi wa zamani uliokuwepo na
kujenga mradi unaotumia teknolojia za kisasa na umeme wa jua, lengo
likiwa ni kuwapatia maji safi na salama maelfu ya wakimbizi kwenye kambi
ya Nyarugusu na maeneo ya vijiji jirani”.
Skibsted, ameongeza kusema kuwa mradi huu ni wa pekee miongoni mwa
miradi ya maji iliyotekelezwa na taasisi hiyo kwa kuwa mbali na
kuwezesha jamii kupata maji safi zinawezeshwa kupata maarifa ya kutunza
mradi na matumizi ya nishati mbadala kuendesha miundombinu yake “Mfumo
wa ushirikiano wa wadau kufanikisha miradi kwa maeneo yenye mahitaji
unapaswa kutumika sehemu mbalimbali duniani kama ambavyo wadau
mbalimbali wameshirikiana kuhakikisha eneo hili la wakimbizi wanapata
maji salama na kuondoa hatari ya milipuko ya magonjwa yatokanayo na
ukosefu wa maji salama”,alisisitiza.
Naye Makamu wa Rais wa miradi ya kimataifa kutoka Water Mission
International, Bw. Seth Womble, amesema kuwa kufanikisha kwa miradi ya
maji katika makambi ya wakimbizi kumewaongezea kujiamini katika
utekelezaji katika maeneo mengine nchini na kanda nzima “Ushirikiano
wetu na wadau wengine unadhihirisha jinsi unavyoweza kufanikisha miradi
kwenye maeneo mengine yenye changamoto maji salama kama ilivyo dira ya
shirika la Water Mission”.
No comments :
Post a Comment