
Waziri Selemani Jafo,akizungumza kwenye ufunguzi wa Teachers day mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na benki ya NMB

Baadhi ya walimu Mkoa wa Dodoma wakishiriki Mkutano uliyoandaliwa na benki ya NMB

Waziri Selemani Jafo akikaribishwa na Meneja wa Kanda ya Kati NMB,Nsolo Mlozi.

Waziri Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja
………………….
Serikali imeitaja benki ya NMB
kuwa miongoni mwa taasisi zilizofanikisha makusanyo ya fedha kwa mwaka
2018/19 kwa kuwa benki hiyo haina tofauti na Wizara ya Tamisemi kwa
kufika maeneo yote nchini.
Kauli hiyo ilitolewa jana na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) Seleman Jafo, wakati
akizungumza
na walimu zaidi ya 300 kutoka halmashauri za wilaya mkoani Dodoma
katika siku ya mwalimu ambao walikutanishwa na benki ya NMB.
Waziri Jafo alisema uamuzi wa
benki hiyo kwenda nchi nzima na kufungua matawi, mawakala pamoja na
kuongeza ATM, ulisaidia kwa watu kuzifikia kwa urahisi huduma za kibenki
pamoja na halmashauri kuitumia kwa makusanyo yake.
Hivi karibuni Jafo alitangaza
mapato ya serikali kutoka katika halmashauri yakipanda kutoka asilimia
73 ya mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 81 mwaka 2018, juzi kwenye za
mapato katika mmalaka ya serikali za mitaa tumekusanya takriban billioni
664 sawa na asilimia 91 kiasi ambacho hakijawahi kufikiwa. Ninyi NMB
mmetusaidia kwa hili,” alisema Waziri Jafo.
Kuhusu benki ya NMB alisema ni
miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri hapa nchini ikiwa na wateja
zaidi ya 3.5 milioni pamoja na matawi 229 ambayo ni zaidi ya halmashauri
zilizopo ingawa aliwataka waongeze wateja na kuagiza kitengo cha
utafiti kufanya kazi yake vizuri.
Kuhusu mikopo alisema kuna kilio
kutoka kwa watumishi kuhusu riba kubwa ya mikopo kwenye mabenki yote
nchini kwani wanatoza kiwango ambacho si rafiki kwa wafanyakazi jambo
linalopekea malalamiko na wengine kujutia uamuzi wa kukopa.
“Naomba suala la riba mliangalie,
haiwezekani riba ya mfanyakazi ikawa sawa na anayefanya biashara, ndiyo
maana mnasababisha walimu kuingia madeni kwenye visaccos vingine hadi
wanaacha kadi zao huko mwisho wa siku wengine wanataka kujinyonga,
tafakarini ikibidi mfike hata kwenye single digit,” alisema Jafo.
Katika hatua nyingine aliwataka
walimu kutumia mishahara yao kwa utaratibu na kuacha maisha ya kuiga
kwani ndiyo yanayowapelekea kwenye madeni makubwa.
Meneja wa NMB Kanda ya kati Solo
Mlozi alisema benki hiyo imejipanga kuwafikia Watanzania mahali walipo
kwa kutumia mawakala wake na kuendelea kuboresha huduma zao kwa kadri
iwezekanavyo.
Mlozi alimwomba Waziri kufikisha
ujumbe wao serikalini ili waendelee kuiamini benki hiyo na kufanya nayo
kazi kwa kuwa serikali ina hisa ya asilimia 31 ndani yake hivyo na mambo
yaliyozungumzwa watashauriana ili kuwapunguzia mzigo Watanzania.
Awali Meneja Mwandamizi wa wateja
wadogo Ally Ngingite alisema benki hiyo imeweka utaratibu kuwafikia
walimu kama sehemu ya wateja na kusikiliza changamoto zao.
Ngingite alisema mpango huo
ulianzia Jijini Dar es Salaam,Pwani na jana Dodoma kabla ya kwenda mikoa
mingine ikiwemo Zanzibar huku akitaja benki kusogeza huduma zaidi kw
akutumia simu za mkononi.
No comments :
Post a Comment