Aliyekuwa ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Safaricom nchini Kenya, Bob Collymore amefariki dunia leo asubuhi, Julai Mosi, 2019.
Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Safaricom,
Nicholas Nganga imesema Collymore alikuwa anasumbuliwa na saratani kwa
muda mrefu.
“Oktoba 2017 alienda Uingereza kwa matibabu na akarejea Julai 2018
kuendelea na majukumu yake huku akihudhuria hospitali kila ilipobidi.
Mara ya mwisho alikuwa anatibiwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga
Khan hapa Nairobi kabla hali yake haijawa mbaya zaidi,” amesema Nganga.
Raia huyo wa Uingereza ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa mjumbe wa
bodi ya taasisi ya saratani nchini Kenya, ameacha mke, Wambui Kamiru, na
watoto wanne.
Kifo cha Collymore (61), kimetokea mwezi mmoja kabla hajastaafu kwani alipanga kuachia wadhifa huo Agosti mwaka huu.
No comments :
Post a Comment