R.I.P AGNES KABIGI
Meneja
Mawasiliano wa asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia
Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Bi. Agnes
Kabigi amefariki dunia leo Ijumaa Julai 26,2019.
Taarifa
za awali zinasema Agnes Kabigi ambaye ni mwandishi wa habari wa... muda
mrefu aliyetumikia vyombo mbalimbali vya habari kuamnzia miaka ya 90
amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla wakati akitekeleza majukumu
yake wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Taarifa
za kifo cha Agnes Kabigi aliyewahi kuwa mwandishi wa gazeti la Nipashe
katika ngazi mbalimbali zimethibitishwa na Mkurugenzi wa Shirika la
AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa.
"Ni kweli ndugu yetu Agnes Kabigi ametutoka,amefariki dunia huko Kahama baada ya kuanguka akiwa kwenye majukumu ya kikazi" - Dkt. Mwakyusa.
No comments :
Post a Comment