Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. William Erio
(kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Banda la Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (wapili kushoto),
pamoja na Afisa Matekelezo wa NSSF, Bi.Diogi Janguo, (wapili kulia) na
Mtaalamu wa mifumo ya computer, NSSF Bi.Grace Magigile wakati Bw. Erio
alipofika kwenye Banda namba 13 ambalo Mifuko yote miwili ya PSSSF na
NSSF inatoa huduma kwa ushirikiano katika jengo hilo. Itakumbukwa kuwa
PSSSF ni Mfuko ulioundwa kuhudumia Watumishi wa Umma na NSSF kuhudumia
Sekta binasi.
Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Donald P. Maeda (kushoto), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko huo.
Afisa
Mwandamizi wa Malipo, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa
Umma,(PSSSF), Bi.Nyangi Masalu (kulia), akiwahudumia wanachama wa Mfuko
huo waliotembelea banda la PSSSF kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar
es Salaam Juni 30, 2019.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kushoto), akiwahudumia wananchi hawa waliofika kwenye banda hilo.
Timu
ya PSSSF ikiongozwa na Mkurugenzi wa Banda la Mfuko huo Bi. Eunice
Chiume ikiwa tayari kutoa huduma bora kwa wanachama na wananchi
watakaofika kwenye banda hilo.NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAONESHO
ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, tayari yamepamba moto
ambapo Mkurugenzi wa Banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa
Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, ametoa wito kwa Wanachama wa Mfuko
huo pamoja na Wananchi kufika kwenye banda hilo ili kupata elimu kuhusu
huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko.
Bi.
Chiume amesema, banda la PSSSF liko Banda namba 13 mkabala na jengo la
matangazo ndani ya viwanja vya Maonesho Sabasaba barabara ya Kilwa
jijini Dar es Salaam.
"Mfuko wa PSSSF umeundwa baada ya kuunganishwa
kwa mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF, PSPF, LAPF
na PPF na kwa sababu hiyo bado ni mpya na wanachama wanahitaji
kuelimishwa kuhusu majukumu mapya ya Mfuko huo kwa wanachama ambao ni
watumishi wa Umma." Alifafanua Bi. Chiume.
Alisema uduma za PSSSF zitatolewa kwenye jingo moja ambalo pia linatumiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Maonesho
hayo yameanza Juni 28 na yatafikia kilele Julai 13, 2019 na kauli mbiu
ya mwaka huu ni "Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa maendeleo endelevu ya
viwanda."
No comments :
Post a Comment