Wednesday, May 1, 2019

NHIF TANGA YATUMIA MAADHIMISHO YA MEI MOSI KUWAKUMBUSHA WAAJIRI KUTOA MICHANGO YA WATUMISHI WAO


 
 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF)
Happines Sima akizungumza wakati wa maadhimisho hayo leo
 Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kushoto ni Meneja wa
Mfuko huo mkoa wa Tanga Happines Sima akiweka sawa mwamvuli wakipita
mbele ya mgeni rasmi
 
 Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF)
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga umetumia maadhimisho ya
siku ya wafanyakazi dunia (Mei Mosi) kuwakumbusha waajiri kuhakikisha

wanatoa michango kwa ajili ya watumishi wao.
Akizungumza wakati
wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya CCM
Mkwakwani mjini Tanga Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga Happines Sima
ambapo aliwataka waajiri kuzingatia suala hilo.
Alisema pia
wametumia fursa hiyo kuweza kuhamasisha waajiri ambao watumishi wao
ambao hawajajiunga na mfuko huo wajiunge ili waweze kunufaika na fursa
zilizopo ndani ya mfuko huo.
“Lakini pia katika maadhimisho haya
tumeweka banda letu ili kuweza kuwasikiliza wafanyakazi na kutatua kero
zao mbalimbali zinazowakabili “Alisema Meneja huyo.
Hata hiyo
aliwataka wazazi na walezi kuwaandikisha watoto wao kwenye mpango wa
Toto Afya Kadi ili waweze kunufaika na huduma ya matibabu pindi
wanapougua .
Mwisho.

No comments :

Post a Comment