Meneja wa QNET wa kusini mwa
Afrika, Biram Fall (kushoto)akiwa amepozi na Mjumbe wa Baraza la
Mawaziri Ofisi ya Rais, Guinea-Conakry, Ndugu Cissé Ibrahim Sory wakati
wa kongamano la QNET la V-Convetion lililofanyika mjini Penang, Malaysia
hivi karibuni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa QNET, Ms.
Malou Calouza(wa kwanza kushoto) na Maofisa wa serikali ya Malaysia
wakikata utepe kuzindua rasmi kongamano la V-Convetion lililofanyika
mjini Penang, Malaysia hivi karibuni. Wengine ni wajumbe wa Bodi wa QNET
……………………
Penang, Malayasia,
Kampuni maarufu ya kimataifa ya
mauzo ya moja kwa moja yenye asili ya Asia, QNET imeendesha kongamano la
siku tano la kimataifa ambalo linaleta pamoja takribani
wajasiriamali
13,000 kutoka maeneo mbalimbali duniani katika kisiwa cha Penang,
Malaysia Takribani wajasiriamali wa kiafrika wenye shauku wapatao 2600
walishiriki katika kongamano la mwaka huu.
Kongamano ambalo hufanywa mara
mbili kwa mwaka la (V-Convention) ni tukio la kipekee ambalo huleta
pamoja wateja na wasambazaji wa QNET kutoka maeneo mbalimbali duniani,
washirika wake wa kibiashara, na pia maofisa wa serikali kuja kujionea
bidhaa na huduma za QNET na kuelewa vyema biashara yake.
Kongamano la siku tano
ilijumuisha mfululizo wa programu za mafunzo, hotuba za uhamasishaji,
kutambulisha bidhaa mpya za mtindo wa maisha wa QNET na matukio ya
burudani. Kivutio kikubwa mwaka huu ni QNET Carnival ambayo ilionyesha
zaidi ya nembo au lebo 30 za bidhaa za QNET katika moja ya maonyesho
makubwa kuwahi kufanywa na kampuni hiyo. Bidhaa mpya zilizozinduliwa
mwaka huu ni pamoja na virutubisho vipya kwaajili ya afya ya wanaume
vinavyoitwa QAlive, na toleo lenye ukomo la saa za kifahari kwaajili ya
kumbukizi ya miaka mitano ya ushirikiano kati ya QNET na klabu ya mpira
wa miguu ya jiji la Manchester (Manchester City Football Club).
Moja kati ya dondoo zilizoshika hisia za watu ni sherehe za mahafali ya
wateja ambao wamekamilisha kozi zao kwa njia ya mtandao kupitia qLean,
bidhaa ya elimu ya QNET, ambayo ni maarufu sana miongoni mwa wateja
katika kanda ya Sahara ya Afrika.
Washiriki vile vile walipewa
fursa ya kusikiliza kutoka kwa wazungumzaji rasmi ambao wameshinda
vikwazo vikubwa na kufanikisha ndoto zao. Farouk Saad Hamad Al-Zuman,
raia wa kwanza wa Saudi Arabia kupanda mlima Everest, na Sparsh Shah,
mvulana mwenye umri wa miaka 15 raia wa marekani mwenye asili ya India
aliyezaliwa na tatizo la mifupa dhaifu (brittle bones), ambaye alipewa
siku 2 za kuishi na madaktari baada ya kuzaliwa, na sasa ni nyota katika
mtandao wa Youtube kwa mtindo wake wa kipekee wa mziki ambao
anaunganisha pamoja muziki wa classical na rap.
Bwana Koné Doupin, Mwakilishi
wa Kujitegemea anayeshiriki katika kongamano hilo la (V-Convention)
kutokea Ivory Coast alisema: “Nina furaha sana kuwa hapa mwaka huu.
Tangu nilipojiunga na QNET miaka kumi iliyopita, sijawahi kukosa
kongamano la -V lolote kwa sababu ni fursa ya kipekee kukutana na
viongozi wetu wa juu, kujifunza kutoka kwao, kukutana na watu kutoka
sehemu mbalimbali na kugundua upekee wa bidhaa mpya. Nina shauku kubwa
ya kujaribu bidhaa mpya ya QAlive, kirutubisho kipya cha wanaume na
kugundua ni jinsi gani kinaweza kuboresha maisha yangu.”
Sherehe za ufunguzi
ziliongozwa na watu mbalimbali maarufu kutoka Malayasia na Asia ya
Kusini Mashariki. Mgeni rasmi kutoka Afrika, Bwana Cissé Ibrahim Sory
vile vile alikuwepo katika sherehe za ufunguzi, Bwana Cissé Ibrahim Sory
ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri kutoka ofisi ya Rais katika Jamhuri ya
Guinea-Conakry.
Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa
QNET aliyeteuliwa, Bi. Malou Caluza alisema: “Matukio kama haya ya
Kongamano (V-Convention) hutupa fursa ya kuwahudumia wasambazaji wetu na
kuwapa fursa ya kuona na kushuhudia mtindo wa Kuishi Kikamilifu
(Absolute Living) ambao inaongoza biashara yetu, Vile vile ni jukwaa
bora la kusherehekea ari ya ujasiriamali ambayo kampuni ya mauzo ya moja
kwa moja kama QNET inachochea kwa mamilioni ya watu duniani kote,
kuwasaidia kuboresha maisha yao na kuchangia katika jamii.”
Akiongeza katika hilo, Meneja
Mkuu wa QNET wa kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Bwana Biram Fall,
alisema: “V-Malayasia inafuata msimu wa kongamano la QNET Expo wa mwaka
2019 wenye mafanikio wenye jina la Kuisi Kikamilifu (Absolute Living),
linaloenda sambamba na kanuni ya kampuni ya mauzo ya moja kwa moja QNET
na falsafa yake ya RYTHM – Jiinue Uweze Kuwasaidia Wanadamu (Raise Yourself to Help Mankind)
Kongamano la mwaka 2019 lilianzia jijini Dar es salaam, Tanzania mwezi
uliopita, kisha likahalia Kumasi, Ghana na sasa nchini Malayasia
kwaajili ya kongamano la kiulimwengu la V-Convention. Baadae nchi
zingine za Afrika zitakuwa wenyeji wa kongamano la Kuishi Kikamilifu (Absolute living expo).”
QNET, inauza reja reja bidhaa
mbalimbali za Afya na ustawi, huduma binafsi na urembo, sikukuu,
utunzaji wa nyumba na kozi kwa njia ya mtandao miongoni mwa nyingi
zingine ambazo zinaboresha maisha ya kila siku ya wateja wake duniani
kote. QNET iliwekwa katika moja kati ya makampuni 100 makubwa na imara
ya MLM (Solid Top MLM Companies) kwa mwaka 2018 na Portal ya habari za
mauzo ya moja kwa moja ya Business for Home.
Katika Afrika Magharibi, Chama
cha Ghana cha CSR (GHACEA) mwaka 2018 kiliitunukia QNET kuwa Kampuni ya
Mwaka ya Biashara ya Mtandao (E-Commerce Company of the Year.)
-Mwisho-
Kuhusu QNET
QNET ni moja kati ya makampuni ya
mauzo ya moja kwa moja kutoka Asia yanayoongoza ambayo inatoa aina
mbalimbali za bidhaa za afya, ustawi na mitindo ya maisha ambayo
yanasaidia watu kuishi maisha bora zaidi. Kwa miaka 20, Mtindo wa
biashara ya kuanzia ngazi ya chini ya QNET umeongezewa kasi na nguvu ya
biashara ya mtandao imesaidia kuwawezesha mamiloni ya wajasiriamali
katika nchi zaidi ya 100 duniani kote.
Makao makuu ya QNET yako Hong Kong
na imefungua ofisi zake katika zaidi ya nchi 25 duniani kote kupitia
kampuni tanzu, ofisi za matawi yake, ushirikishaji wa mawakala na
uwakala.
QNET ni mwanachama wa Chama cha
wauzaji wa moja kwa moja (Direct Selling Association) cha Malayasia,
Singapore, Ufilipino, Indonesia na UAE, pamoja na Chama cha Chakula Bora
cha Hong Kong (Hong Kong Health Food Association) na Chama cha viwanda
vya Virutubisho vya afya cha Singapore (Health Supplements Industry
Association) miongoni wa vingine.
QNET pia inafanya vizuri katika
udhamini wa michezo duniani. Baadhi ya ushirikiano mkubwa inajumisha
kuwa mshirika wa mauzo wa moja kwa moja wa Klabu ya Mpira wa miguu ya
Manchester (Manchester City Football Club) na Shirikisho la Soka Afrika
(CAF), Ligi ya Mabingwa ya Total ya CAF, Kombe la Shirikisho la Total
CAF na Kombe la Total CAF Super Cup kwa mwaka 2018 na 2019.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea:
Tovuti ya QNET kupitia: www.qnet.net
Blogu ya QNET Afrika kupitia: www.qnetafrique.com
No comments :
Post a Comment