Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), nchini leo tarehe 1 Mei, 2019, katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es salaam. Mazungumzo hayo yamejikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na EU hususan katika nyanja za elimu na udhibiti wa biashara haramu ya dawa za kulevya.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (Mb.), akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo. |
Kaimu Balozi Stuart akielezea jambo wakati wa mazungumzo hayo. |
Afisa Mambo ya Nje wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Albert Philipo akifuatilia mazungumzo hayo. |
Juu na chini mazungumzo yakiendelea. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (Mb.) akiagana na Kaimu Balozi Charles Stuart mara baada ya mazungumzo. |
No comments :
Post a Comment