Mratibu
wa TIMUN 2019, Kevin Edward akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki
(hawapo pichani) wakati wa mkutano kivuli wa Baraza la Umoja wa Mataifa
(TIMUN2019) ulioanza kuunguruma jana mjini Morogoro.
Afisa
wa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Nafisa
Didi akifungua rasmi mkutano wa kivuli WA Baraza la Umoja wa Mataifa kwa
niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa ulioanza kuunguruma jana
mjini Morogoro.
Baadhi
ya vijana wanaoshiriki mkutano kivuli wa Baraza la Umoja wa Mataifa
(TIMUN 2019) kutoka nchini mbalimbali unaoendelea kuunguruma mjini
Morogoro.
Picha
ya pamoja ya makundi ya vijana wanaoshiriki mkutano kivuli wa Baraza la
Umoja wa Mataifa unaoendelea kuunguruma mjini Morogoro.
MKUTANO
kivuli wa Baraza la Umoja wa mataifa (TIMUN2019) umeanza Jana tarehe
29/4/2019 katika mji wa Morogoro, kiasi cha kilometa 192 kutoka mji wa
kibiashara wa Dar es salaam.
Mkutano
huo ambao unahudhuriwa na vijana 200 kutoka duniani kote unafanyika
chini ya kaulimbiu “Sauti za Vijana kwenye Malengo ya Maendeleo
Endelevu: Uwezeshwaji Ujumuishwaji na Usawa.”
Afisa
wa Habari katika kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.
Nafisa Didi akizindua rasmi mwanzo wa mkutano kwa niaba ya Mwakilishi
Mkazi wa Umoja wa Mataifa alihimiza vijana kutumia vizuri muda wao
katika mkutano huu wa siku tano na kuonyesha vipaumbele vinne muhimu vya
kujadiliwa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu ya dunia (SDGs).
Mkutano
huo mkubwa unaendeshwa kwa mfano wa mfumo wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa, kisheria na kikanuni. Mkutano huo unatambuliwa kimataifa kama
Tanzania International Model United Nations (TIMUN) 2019 unajumuisha
vijana kuanzia miaka 15-30.
Kwa
mujibu wa taarifa majadiliano katika mkutano huo yatalenga zaidi
ushiriki wa vijana katika kipengele cha tatu cha SDG kinachogusa Afya na
ustawi; Kipengele cha nane kazi zenye staha na ukuaji wa uchumi;
kipengele cha 13 mabadiliko ya tabia nchi na kipengele cha 16 cha amani,
haki na kuwa taasisi zenye uwezo .
TIMUN
inaendeshwa na Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA), na hufanyika kila
mwaka kwa vijana kuletwa pamoja kutoka mataifa mbalimbali duniani .
Tukio
la mwaka huu limedhaminiwa na Umoja wa Mataifa Dar es salaam, ofisi ya
Waziri Mkuu, UNICEF, UNFPA, UNIC, Ubalozi wa Marekani, Pathfinder, Plan
International na International Youth Foundation.
No comments :
Post a Comment