Tuesday, April 2, 2019

KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA DC MURO


index
Kamati ya Bunge, Mifugo, Kilimo na Maji imempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro kutokana na mkakati wake wa kukwama miradi ya maji iliyokwama kwa muda mrefu katika wilaya hiyo.
Hayo yamejiri kwenye ziara ya kamati hiyo wilayani Arumeru Mkoani Arusha baada ya kamati ya Bunge Mifugo, Kilimo na Maji kufanya ziara yakukagua miundo mbinu ya miradi mikubwa ya maji ya vijiji 10 inayoendelea kujengwa yenye lengo la kuondoa changamoto ya
uhaba wa maji safi na salama .
Akizungumza mara baada ya kukagua Miradi hiyo ya Maji Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Eng. Emmanuel Kalobelo amesema amefurahishwa na kitendo cha Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Muro ya kuwasaidia wakandarasi kupata vifaa vya ujenzi yakiwemo mabomba makubwa ya maji kwa dhamana ya ofisi yake kwa wenye viwanda uku taratibu za malipo zikiendelea hatua inayosaidia miradi hiyo kukamilika kwa wakati
“Nashukuru kwa maelezo ya Mhe. Mkuu wa Wilaya ambaye tangu asubuhi ameonyesha jinsi gani anavyofuatilia miradi yote ndani ya wilaya yake, na anafahamu takwimu zote za miradi na stegi zilizofikiwa hivyo Mimi kama mtu wa sekta ya maji nimefarijika kweli na uongozi wa Wilaya ya Arumeru.” Alisema Naibu Emmanuel Kalobelo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo ya bunge Ndugu Mahamoud Mgimwa amesema DC Muro anaitaji pongezi na kuungwa mkono kutokana na juhudi zake anazoonyesha zakuwaletea wananchi wake maendeleo kwa kufuatilia miradi kila hatua , pamoja na kuhakikisha wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya miradi wananufaika kwanza *, hatua ambayo amesema inadhihirisha kuwa *Dc Muro hakai ofisini na badala yake anatumia muda mwingi katika kutembelea miradi
“Mhe Muro hapa anafanya kazi nzuri kuna kazi nyingine ambazo so za kwake lakini anajitolea,naomba tumpongeze sana, unawezajiuliza anafanya kwa ajili ya nani? Lakini ameamua kufanya kwa ajili ya kuwasaidia nyinyi ndugu zake, kwa zile juhudi anazozifanya mkuu wa wilaya na waombeni sana mumuunge mkono.” Alisema Mahamoud.
Kamati hiyo pia ilipata fursa ya kutembelea Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji * mifugo kwa njia ya chupa NAIC Kilichopo Wilayani Arumeru. ambapo walijionea kazi zinazofanywa za kutengeneza mbegu za Ng’ombe wa kisasa wa maziwa na nyama .

No comments :

Post a Comment