Daktari Bingwa wa
magonjwa ya moyo ya watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz
Majani (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
Taasisi hiyo na washindi wa kwanza wa Km. 21 mara baada ya kumalizika
kwa mashindano ya mbio za Heart Marathoni zilizofanyika jana jijini Dar
es Salaam. Lengo la mbio hizo ni kuchangisha fedha kwa ajili ya upasuaji
wa moyo kwa watoto ambapo fedha zilizopataikana zitafanya upasuaji kwa
watoto 50 kuanzia tarehe 7/5/2019.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo
ya watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani (kulia)
akiwa na bibi yake Magreth Mngofi (kushoto) mara baada ya kumaliza
kukimbia mbio za Heart Marathoni zilizofanyika jana jijini Dar es
Salaam.Dkt. Naiz alikimbia
umbali wa Km. 10 na Bibi Magreth alikimbia
umbali wa Km. 5.
……………..
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo ya watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani amechaguliwa kuwa mfanyakazi bora wa Taasisi kwa mwaka 2019.
Dkt. Naiz amechaguliwa na Kamati ya kuchagua mfanyakazi bora kwa kuangalia utendaji
wake wa kazi katika kutoa huduma ya matibabu ya moyo kwa watoto, bidii
ya kazi , kufanya kazi kwa kujituma na kufanya kazi kwa uvumilivu. Pia
ushirikiano mzuri baina yake na wafanyakazi pamoja na uongozi wa Taasisi.
Mfanyakazi
huyu bora wa mwaka 2019 atapewa zawadi ya fedha taslimu shilingi
milioni tatu, cheti na ngao ya kutambua mchango wa kazi anazozifanya.
Fedha hizo atakabidhiwa mkoani Mbeya na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni mgeni rasmi katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zitakazofanyika tarehe 01/05/2019
No comments :
Post a Comment