Friday, March 29, 2019

WASHINDI 15 WAPATIKANA PROMOSHENI YA TIA KITU,PATA VITUZ NA DStv!


Picture 1 Draw
Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (Kushoto) Akizungumza wakati wa droo ya tano ya Promosheni ya Tia Kitu pata vituz, Kulia ni Afisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Jehud Ngolo.   Promosheni hiyo ni ya muda wa wiki 8 ambapo jumla ya washindi 120 watapatikana.
Picture 2 Draw
Mkuu wa Uhusiano MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (Wa pili kushoto) akiongoza droo ya kupata washindi wa wiki ya 5  katika promosheni ya Tia kitu pata vituz ya DStv . Kulia Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Jehud Ngolo , kushoto ni Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania akifuatiwa na Benson Urio wa kitengo cha Teknohama cha DStv. Promosheni hiyo ni kwa wateja wanaolipia kwa wakati kabla vifurushi vyao havijakatika hivyo kupata fursa ya kushinda kifurushi cha miezi miwili. Promosheni hiyo ni ya muda wa wiki 8 ambapo jumla ya washindi 120 watapatikana.
……………….
Dar es Salaam Machi 28, 2019. Kampuni ya inayoongoza kwa huduma bora za vinga’muzi nchini, DStv  imetangaza washindi 15 wa droo ya 5 ya Promosheni hiyo ya wiki nane inayoendelea nchi nzima maarufu kama “ Tia Kitu pata vituz”.
Promosheni hiyo ni ya wazi kwa wateja wote wa DStv ambao watalipia vifurushi vyao kabla
havijakatika. “Mteja yeyote wa DStv atakayelipia kifurushi chake kabla hakijakatika moja kwa moja anaingia katika droo na fursa ya kujishindia kifurushi chake kwa muda wa miezi miwili.” Alieleza Mkuu wa Uhusiano MultiChoice Tanzania Johnson Mshana wakati akiendesha  droo ya wiki ya nne ya promosheni hiyo.
Akizungumza  baada ya kufahamishwa juu ya ushindi wake huo Bw. Yohana Francis ambaye ni mteja wa DStv aliyepo mkoani Mbeya alisema kuwa amefurahi sana kuibuka mshindi na kuongeza kuwa anaishukuru sana DStv na kuwaasa kuwa waendelea kuwajali wateja wake hivyo hivyo.

No comments :

Post a Comment