Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Dkt. Edmund Mndolwa (kulia)
wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika
ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla
ya Uzinduzi wa Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa
Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi Akaunti
ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini
Dar es Salaam.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
…………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu
ya Tano imefanya jitihada kubwa kuweka mazingira mazuri ya
kisera na
kimifumo ili kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha hapa nchini.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Akaunti ya TABASASMU, iliyozinduliwa leo
na Benki ya Posta jijini Dar es Salaam.
“Serikali kupitia Benki Kuu ya
Tanzania imeendelea kutoa miongozo mbalimbali ili kuhakikisha watanzania
takribani asilimia 50 wanafikiwa na huduma za kibenki ifikapo Mwaka
2025”alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amependezwa na wazo la kuhakikisha kuwa kupitia akaunti ya TABASAMU wanawake watauziwa bima za kijamii.
Benki ya Posta ina matawi takriban
80, ATM 54, mtandao wa Umoja Switch takriban 200 na mawakala 150
kupitia Shirika la Posta ambapo Makamu wa Rais ameitaka benki hiyo
kuwafikia wanawake wengi haswa vijijini na kuhakikisha wanapata huduma
na elimu ya masuala ya kifedha.
Makamu wa Rais amesisitiza
kuwa wanawake ni nguzo kuu ya uchumi wetu, kwani wao ndiyo wazalishaji
wakuu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa. Mbali ya kulea familia,
huwezi kuwakosa wanawake kwenye sekta yoyote ya uzalishaji mali, na
hivyo siyo upendeleo kuanzisha akaunti maalumu ya TABASAMkwa wanawake,
bali ni haki yao ya msingi kama ilivyofanya benki ya TPB.
Makamu wa Rais amewataka Akaunti
ya TABASAM inashirikiana na makampuni ya simu kuhakikisha kuwa wanawake
hawa si tu wanapata taarifa za kibenki hata ikiwezekana kuweza kupata
huduma za kibenki kama mikopo kupitia simu zao za mikononi.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema Tanzania ina rekodi nzuri
Afrika na duniani kwa ujumla katika masuala ya huduma za kifedha
No comments :
Post a Comment