Monday, February 4, 2019

NDITIYE AKABIDHI KOMPYUTA SHULE ZA SEKONDARI MPANDA


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akikabidhi kompyuta kwa Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (wa pili kulia) kwa ajili ya shule za sekondari mjini humo. Wakishuhudia, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela (wa pili kushoto)

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa viongozi wa Mkoa wa Katavi, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na waalimu wa sekondari (hawapo pichani) kuhusu ukuaji na maendeleo wa sekta ya Mawasiliano nchini. Kulia kwake ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard akitoa maelezo ya kompyuta walizotoa kwa shule za sekondari za Mpanda. Walioketi wakimsikiliza, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na  katikati ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi

Afisa Elimu wa Shule za Sekondari wa Manispaa ya Mpanda, Enelia Lutungulu akisoma risala ya shukrani kwa Serikali kwa niaba ya waalimu na wanafunzi wa shule kwa kuzipatia shule hizo kompyuta 25. Walioketi wakimsikiliza wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na  katikati ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi

Waalimu wa shule za sekondari, viongozi na watendaji wa mkoa wa Katavi na Manispaa ya Mpanda wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati akiwahutubia kabla ya kukabidhi kompyuta kwa ajili ya shule za sekondari za Mpanda

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akisisitiza jambo kwa Afisa Usalama Msaidizi wa Uwanja wa Ndege wa Katavi, Fredrick Valentine(wa kwanza kulia) wakati akikagua miundombinu na hali ya uwanja huo akiwa ziarani mkoani humo. Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (wa tatu kulia) akifuatilia kwa makini mazungumzo hayo


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyesimama mbele amefunga mikono) akiwa kwenye picha ya pamoja na waalimu wa shule za sekondari, viongozi na watendaji wa mkoa wa Katavi na Manispaa ya Mpanda. Wan ne kulia ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi na wa tano kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela

No comments :

Post a Comment