Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akimkabidhi Magdalena Makalla
(akiwa wodi ya wazazi) neti na mashuka kwa niaba ya Serikali kutoka kwa
kampuni ya Halotel kwa ajili ya Hospitali ya Makole, Dodoma. Wa kwanza
kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Halotel, Nguyen Van Son na wa pili
kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. George Matiko
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akikabidhi
vifaa mbali mbali vya hospitali kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Makole,
Dodoma Dkt. George Matiko (wa pili kulia) kwa niaba ya Serikali kutoka
kwa kampuni ya Halotel kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa. Wa kwanza
kushoto ni Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizarani Mhandisi Dkt. Maria
Sasabo na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Halotel, Nguyen Van Son
wakishuhudia
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akishuhudia
makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 20.6 kwa Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Dkt. Binilithi Mahenge (wa kwanza kulia) kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji Halotel, Nguyen Van Son (wa tatu kushoto) kwa ajili ya
kuanzisha kiwanda cha kufyatua matofali cha kikundi cha vijana, Dodoma
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiongea na wananchi wa Dodoma
kabla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 20.6 kwa Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Dkt. Binilithi Mahenge (hayupo pichani) kwa ajili ya mradi wa
kufyatua matofali wa kikundi cha vijana, Dodoma
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) kwa niaba ya
Serikali akikabidhi moja ya kitanda kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Makole, Dodoma Dkt. George Matiko (wa pili kulia) kutoka kwa Halotel kwa
ajili ya kuhudumia wagonjwa. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Halotel,
Nguyen Van Son
………………………………………………………………………………………………
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amezitaka kampuni za simu za
mkononi nchini kurudisha faida kwa jamii ambayo ni wateja wake na
wanatumia huduma za mawasiliano za kampuni zao
Nditiye ameyasema hayo wakati
akikabidhi vifaa mbali mbali vya hospitali kwa ajili ya kuhudumia
wagonjwa ikiwemo vitanda, neti, mashuka na aproni vyenye thamani ya
zaidi ya
shilingi milioni sita kwa niaba Serikali kwa Hospitali ya
Makole iliyopo Dodoma vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya
Halotel
“Nitoe wito kwa kampuni nyingine za simu za mkononi ziige mfano wa Halotel wa kurudisha shukrani kwa wananchi,” amesema Nditiye
Pia ameongeza kuwa mawasiliano ni
moja ya Sekta ambayo inashika nafasi ya tano kwa maswali Bungeni
ikiwemo Sekta nyingine za maji, afya, elimu, umeme, barabara ambapo
Wabunge wamekuwa wakiuliza maswali mara kwa mara kuhusu Sekta ya
Mawasiliano ambapo inadhihirisha kuwa wananchi wanatambua na kuthamini
mchango wa mawasiliano katika maisha yao ya kila siku kwa kuwa
mawasiliano ni uchumi na ni maendeleo
Vile vile amezitaka kampuni za
simu za mkononi nne zilizosaini mkataba na kupewa ruzuku na Serikali
kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mwezi Desemba mwaka jana
ikiwemo Vodacom, TIGO, Halotel na Shirika la Mawasiliano Tanzania
kujenga minara ya na kupeleka huduma za mawasiliano haraka kwa wananchi
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Makole, Dodoma Dkt. George Matiko akipokea misaada hiyo ameishukuru
kampuni hiyo na kusema kuwa anaipongeza kwa kuunga mkono jitihada za
Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli za
kuboresha sekta ya afya kwa kujenga vituo vya afya nchi nzima na
kuongeza fedha za kununua dawa, vitendanishi na vifaa tiba ambapo hadi
sasa hospitali hiyo imepokea shilingi milioni 500 kutoka Serikalini
ambapo zimewezesha ukarabati wa hospitali hiyo na kuongeza utoaji huduma
kwa wanawake 2,000 waliojifungua na kufanya operesheni kwa wagonjwa 300
“Tunashukuru kwa jitihada zenu
Halotel, mahitaji bado ni mengi, muendelee kutuunga mkono katika
kuwahudumia wananchi,” amesisitiza Dkt. Matiko
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Halotel, Tanzania Nguyen Van Son amesema kuwa wameamua kurudisha faida
na kutoa shukrani kwa wananchi kwa kuwaunga mkono kwa kutumia huduma za
kampuni yao ambayo imesambaa nchi nzima na inatoa huduma kwenye maeneo
yote ya mijini na hasa vijijini
Nguyen ameishukuru Serikali kwa
kuweka mazingira wezeshi na rafiki yaliyowavutia kuweza nchini kwenye
Sekta ya Mawasiliano na wamedhamiria kuendelea kushirikiana na Serikali
na wananchi kwa ujumla ili kupanua huduma za mawasiliano na kuhakikisha
kuwa zinakuwa za viwango, ubora na gharama nafuu kwa mtumiaji
Katika hatua nyingine, Nditiye
kwa niaba ya Serikali, ameshuhudia makabidhiano ya hundi ya shilingi
milioni 20.6 baina ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilithi Mahenge na
Nguyeni kwa ajili ya uanzishaji wa kiwanda cha kufyatua matofali cha
kikundi cha vijana wa Dodoma ambapo makabidhiano hayo yamefanyika kwenye
viwaja vya Barafu mjini humo
“Vijana wa Dodoma mtanufaika na
Serikali kuhamia Dodoma, tumeona tuanzishe kikundi cha vijana ili waweze
kuanzisha kiwanda cha kufyatua matofali na mradi huo utakuwa na vijana
wa kutoka Jeshi la Kujenga Taifa ili wawasaidie ili baadae vijana waweze
kuanzisha na kuendeleza viwanda vyao,” amesema Dkt. Mahenge
Pia, ametoa rai kwa vijana
wajitokeze na kuchamkia fursa mbali mbali zilizopo mkoani humo na
wasikubali kukaa bure, wajihusishe na shughuli za uzalishaji, wasikubali
kukaa nyumbani na vijiweni
No comments :
Post a Comment